Header Ads Widget

UVCCM MOSHI VIJIJINI WAJA NA OPERESHENI 'KATA KWA KATA

 

Na Gift Mongi MATUKIODAIMA App,Moshi.

Ni mwendo wa kata kwa kata katika wilaya ya Moshi Vijijini zoezi linalotekelezwa na mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM)Yuvenail Shirima


Lengo la ziara hii ni kuimarisha uhai wa jumuiya hiyo lakini pia kujenga misingi iliyo bora kwa wanachama wa chama cha mapinduzi(CCM) na wafuasi wake kiujumla.


Aidha Shirima akiwa ziarani alipitia vijana wajasiriamali na kuzungumza nao kwa kusikiliza kero zao pia kuwaungisha kwenye biashara zao.  

'Nimekuja hapa lengo ni kuona shughuli ambazo vijana wenzangu mnazifanya na nimefurahi sana na hapa inaonyesha ni jinsi gani hamsubiri ajira ila mnajishughulisha'anasema


'Niseme tu kuwa CCM ambao ndio chama dola kina dhamira halisi katika kuwasaidia vijana na kuwa kinachoonekana ni mwendelezo wa mawazo mema kama vijana katika kujikwamua kiuchumi'anasema

Doris Mtey mkazi wa kata ya Kilema Kusini anasema ziara za umoja huo wa vijana zinaleta faraja kwa vijana wenzao kwani zinawapatia fursa za kiuchumi.


'Wanakutana vijana tofauti tofauti na kuwa hii inaleta maono mapya kwa wale ambao wanataka kujiajiri lakini hata kukiimarisha chama chenyewe'anasema


Kamati ya utekelezaji chini ya mwenyekiti Yuvenali Shirima wako kwenye ziara za kata hadi kata kuimarisha jumuiya na chama. 


'Yaani tumejipata tumeachilia breki speed 220 No Touch wembe ni ule ule kazi iendelee'anasema mwenyekiti huyo wa UVCCM wilaya ya Moshi Vijijini

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI