Na Fatma Ally, Matukio DaimaApp, Dar
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Hussein Ali MwinyI amesema Tanzania imepiga hatua katika kuongeza upatikanaji wa huduma fedha kwa wanawake kwani kumekuwa na ongezeko kubwa la wanawake wenye kutumia huduma za kibenki kutoka asilimia 66 mwaka 2017 hadi asilimia 80 mwaka 2023.
Aidha, amewataka mawaziri wa fedha na mawaziri wa maendeleo ya jamii katika nchi za Afrika kuimarisha mipango ya maendeleo ili kuimarisha haki za kiuchumi za wanawake katika Bara zima la Afrika.
Rai hiyo ameitoa leo jijini Dar es salaam wakati akifungua mkutano wa mawaziri wa Afrika kuhusu uwekezaji kwa maendeleo ya usawa wa jinsia.
Amesema kuwa, sera zote za ubaguzi wa kijinsia zinapaswa kuondolewa na kupitisha utekelezaji wa sheria na sera na kuweka mikakati ya uwekezaji ili kuwezesha upatikaji wa haki za wanawake na wasichana.
Aidha, ameongeza kuwa mabadilko ya tamaduni yanapaswa kuingiliwa ili kubadilisha kanuni za kijamii zinazoleta au kuchochea ubaguzi.
Amesema kuwa, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejitolea kushughulikia kukosekana kwa usawa wa kijinsia kwa vitendo katika nyanja zote za mwanamke.
"Kipengele cha jinsia kimejumuishwa kikamilifu katika mpango wa taifa wa maendeleo wa miaka mitano(2021/22-2025/26)na dira ya maendeleo ya Tanzania 2025 ambayo yote yanasisitiza dhamira ya nchi katika kukuza usawa wa jinsia katika kijamii,kiuchumi na kisiasa"amesema Dkt Mwinyi
Ameongeza kuwa “Mafanikio haya ya ushirikishwaji wa kifedha kwa wanawake ni matokeo ya kuongezeka kwa utoaji wa namba ya vitambulisho vya taifa kwa wanawake na bidhaa za kifedha sasa zinafukiwa na wanawake”amesema.
Kwa upande wake, Waziri ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu,Dkt Dorothy Gwajima amesema kuna haja kubwa ya kuwekeza kwenye jinsia ili kuisaidia Serikali kutotumia fedha nyingi kwenye mapambano ya jinsia badala yake fedha hizo zipelekwe kwenye mahitaji ya kijamii.
Amesema kuwa, maswala ya ukatili wa kijinsia yanayofanywa kutokana na Mila na desturi yanarudisha nyuma maendeleo ya wanawake ambao wanamvhango mkubwa kwenye maendeleo ya sekta zote.
"Kwa kuacha hizi tabia kandamizi zitasaidia hizi fedha tunazotumia katika kupambana na ukatili zikaongezwa kwenye maendeleo na swala la ukatili si swala la Tanzania tu ni swala la bara zima la Afrika"
Aidha amempongeza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kupiga hatua katika kuendeleza na kuwekeza kwenye maswala ya kijinsia kwani sasa hivi idadi kubwa ya viongozi nafasi ya mwanamke ipo na inafanya vizuri.
Naye,Waziri wa Fedha Dkt Mwigulu Nchemba amesema kuwekeza kwa wanawake ni kichocheo kikubwa cha uchumi katika nchi hivyo serikali itaendelea kuwawezesha na kutunga sera zitakazosimamia mopango na maendeleo endelevu.
Naye, Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki UN Women Dkt. Maxime Houinato amesema mawaziri wa fedha wanahitajika kuangalia namna bora ya kuwawezesha wanawake.
Aidha Dkt. Houinato ametoa rai kwa serikali na sekta binafsi kuhakikisha mabinti wanapotoka chuo wasaidiwe kupata kazi ili kuepuka kuingia kwenye ukatili.
Amesema kuwa, Shirika la UN Women kwa kushirikiana na nchi wanachama litaongeza ufadhili katika masuala ya usawa wa kijinsia ili kuwawezesha wanawake na wasichana kutoka nchi wanachama kwa kuwaunganisha na wafadhili ili kuharakisha maendeleo ya kundi hilo.
0 Comments