SERIKALI ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa imesema itawachukulia hatua kali wazazi wa wanafunzi watakaobainika na mimba pindi shule zitakapofungua mwakani 2024.
Kuwa hivi karibuni shule zote na msingi na sekondari zinakwenda kufungwa kwa ajili ya wanafunzi kwenda rikizo ndefu ya mwezi zaidi ya mmoja hadi hapo mwakani kama itakapotangazwa na wizara husika hivyo kwa kuwa hadi sasa wanafunzi wamelelewa vyema shuleni kwa kuwa salama pasipo kuwa na mimba ni vizuri wazazi kuwalinda watoto wao kwa muda ambao wakakuwa nao nyumbani wakati wa likizo.
Mkuu wa wilaya ya Mufindi Dkt Linda Selekwa aliyasema hayo juzi wakati wa mahafali ya nane katika chuo cha ufundi standi Rural Development Organization (RDO) Mdabulo alisema hadi hivi sana kwenye tarafa ya Ifwagi hakuna taarifa ya mimba za wanafunzi mashuleni jambo ambalo linaonesha kwa kiasi kikubwa jinsi ambavyo walimu walivyowewza kulinda vema watoto kwa wakati wote wa masomo shuleni.
Hivyo ni wajibu wa wazazi kuhakikisha wakati huu wa likizo ndefu ya mwisho wa mwaka wanabeba dhamana ya kulinda watoto wao ili shule zitakapofunguliwa watoto hao warudi mashuleni wakiwa salama bila ya mimba.
Alisema hadi sasa pamoja na kata ya Mdabulo na Ifwagi kutokuwa na taarifa za mimba za wanafunzi ila kuna baadhi ya maeneo kwenye kata na tarafa nyingine zimekuwepo taarifa za mimba za wanafunzi na wahusika wote wa mimba hizo wamekwisha chukuliwa hatua kwa kufikishwa mahakamani .
Hivyo alisema kama serikali ya wilaya isipenda kuona wanafunzi wanakatishwa ndoto zao na masomo kutokana na mimba na kuwa wahusika wa mimba za wanafunzi hawatafumbiwa macho na hata kama mwalimu atabainika kuhusika atachukuliwa hatua kali za kisheria.
" Ninachowaomba wazazi kuwalinda watoto wetu na kutowaficha wale wanaosababisha watoto wetu kutotimiza ndoto zao na kupata elimu wafichueni wahusika na mimba ila sheria ichukue mkondo wake hakuna haja ya kuwaficha hao sil watu wema hata kidogo ikibainika mzazi umemficha mhusika wa mimba za wanafunzi wewe ndio utabeba dhamana ya kufikishwa mahakamani " alisema
Dkt Selekwa ambae ndie alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo aliwakilishwa na katibu tawala wa wilaya ya Mufindi Frank Sichalwe alisema kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameendelea kugharamia elimu bila malipo lengo kuwezesha kila mtoto wa mtanzania kupata elimu pasipo kisingizio cha kukosa ada .
Kuwa kutokana na jitihada hizo za Rais Dkt Samia ni vizuri kila mmoja wetu kuunga mkono kwa kuhakikisha hakuna mtoto anyekatishwa masomo kwa kisingizio chochote na wale wanaosababishiwa kukatisha masomo kwa sababi zinazozuilika za mimba basi waliohusika na sababu hizo wanapaswa kuwajibishwa vikali .
Pia alisema hata kwa wanafunzo wanaosoma vyuo mbali mbali zikiwemo vya ufundi pia wanapaswa kulindwa dhidi ya mimnba ili kutimiza ndoto zao za kumaliza mafunzo salama kwani alisema pamoja na serikali kugharamia elimu ya msingi na sekondari imekuwa ikigharamia elimu ya vyuo vya ufundi kwa kufadhili masomo ya muda mfupi kwa wanafunzi wenye uhitaji na shabaha ni kuona vijana wenye ndoto ya kuja kuwa mafundi wanawezeshwa hivyo si sawa kama ndoto zao zitavurugwa na mtu .
Katika hatua nyingine alisema kuwa serikali wilayani Mufindi imeendelea kuweka mfumo mzuri wa wakulima kupata mbole ya Ruzuku kwa wakati na tayari mbolea zimeanza kusambazwa ili kuwezesha wakulima kutumia mvua zinazotarajia kuanza kunyesha kwa kilimo .
Alisema ni wajibu wa kila mmoja kuanza maandalizi mapema ya mashamba na kwa wale vijana wanaoshinda vijiweni wanapaswa kutambua kuwa kufanya hivyo ni kosa na iwapo watakutwa vijiweni muda wa kazi watawajibishwa pia .
Akizungumzia kazi mbali mbali zinazofanywa na chuo hicho cha RDO Mdabulo alisema kuwa kwa upande wa serikali ya wilaya ya Mufindi inathamini mchango mkubwa wa chuo hicho hasa katika kuhudumia jamii inayokizunguka chuo kwa kuanzisha miradi ya maji safi na salama pia vijana kuwa na ujuzi mkubwa wa kutengeneza bidhaa mbali mbali .
Hivyo kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za chuo serikali ya willaya ya Mufindi itaendelea kuhimiza wazazi kulipa ada kwa wakati pia kuona inaunga mkono jitihada za chuo hicho kwa kununua bidhaa zinazozalishwa na wanafunzi hao zikkiwemo batiki na bidhaa nyingine .
Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa RDO Fidelis Filipatali mwakilishi wa mkurugenzi huyo Obadia Ngailo alisema kuwa chuo hicho kimefanikiwa kusajili wanafunzi wa kozi za muda mfupi wapatao 42 wavulana 31 na wasichana 11 pia kusimamia nidhamu ya wanafunzi na watumishi na kuchukua hatua stahiki inapojitokeza masuala ya utovu wa nidhamu.
Pia wamefanikiwa kuongeza vyanzo vya uzalishaji mfano nyuki, na ng’ombe wa maziwa, hivyo kuongeza pato la chuo na kuongeza ufanisi kwa wanafunzi wa fani ya kilimo na ufugaji ,wamefanikiwa kuhamasisha wanafunzi kufanya kazi za mikono kwa ajili ya kujifunza kwa vitendo zaidi na kuongeza kipato cha idara.
"Tumefanikiwa kununua shamba la idara lenye takribani ekari 60 kwa mapato ya ndani ya idara ili kuendesha shughuli za ufugaji na kilimo tumefanikiwa kuanzisha mgahawa kwa ajili ya watumishi na wanafunzi ili kutoa huduma ya chakula na kuongeza mapato ya idara pia kuongeza ujuzi kwa wanafunzi wa upishi na wamefanikiwa kupata tenda mbali mbali toka jamii inayotuzunguka na tenda za serikali kama vile kujenga Zahanati, madarasa, kutengeneza madawati na kuandaa vyakula vya wageni mbali mbali katika maeneo yanayotuzunguka "
Ngailo alisema kuwa wamefanikiwa na tunaendelea kuandaa na kufanya semina na warsha mbali mbali kwa watumishi na wanafunzi wa vyuo vyetu, zikiwemo semina za ujasiriamali mifumo wa ufundishaji na warsha inayohusu matumizi bora ya ardhi (PERMACULTURE)Kwa kushirikiana na ofisi ya TEHAMA.
Alitaja changamoto zinazokabili chuo hicho kuwa ni Kukosekana kwa nyumba za watumishi hali inayofanya baadhi ya watumishi kutembea umbali mrefu na wengine kuishi mazingira ambayo si mazuri pia kukosa viwanja vya michezo mbali mbali kama vile, mpira wa miguu, mpira wa pete pamoja na Uhaba wa madarasa hasa kwa fani ya ujenzi na ufundi magari.
MWISHO
0 Comments