![]() |
| Mkuu wa mkoa wa Njombe Mhe. Antony Mtaka akizungumza na wanafunzi wa Mabatini sekondari mjini Njombe kuelekea mtihani wa mwisho wa kidato Cha nne |
Na Gabriel Kilamlya Matukio Daima APP NJOMBE
Mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka amesema mzazi atakayegoma kumpeleka shule mtoto aliyefaulu kwenda sekondari atahama mkoa kwani hataki mchezo katika suala la elimu.
Mtaka ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanafunzi wa mabatini sekondari mjini Njombe wakati akiwatakia mtihani mwema wanafunzi wa kidato Cha nne unaotarajiwa kuanza Novemba 13 mwaka huu.
Aidha amesema hataki kusikia mzazi kagoma kumpeleka shule mtoto katika mkoa wa Njombe kwani hatua kali zitachukuliwa kwa atakaye kaidi suala la elimu kwa mtoto.
Hata hivyo Wazazi mkoani Njombe wametakiwa kuwapunguzia kazi wanafunzi wanaojiandaa na mitihani ya taifa ya kidato cha nne ili watumie muda mwingi kujisomea katika dakika za mwisho.








0 Comments