Header Ads Widget

RC MBEYA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA CHANZO CHA VIFO

 


Na .Matukio Daima Media,Mbeya

MKUU wa Mkoa wa Mbeya,Juma Homera amesema  kuwa asilimia kubwa ya wananchi wanapoteza maisha kutokana na magonjwa yasiyoambukiza ,msonga wa mawazo

Kutokana na hali hiyo ,Homera amehamasisha wananchi kuwa na utamaduni wa kufanya mazoezo ili kujenga afya ya mwili ,kuondoa mawazo na kuoshi kwa furaha .


Homera amesema hayo leo  wakati akifungua ,bonanza la Siku ya wanafamilia 2023 kwa Watumishi wa Hosptali ya Rufaa Kanda ya Mbeya (MZRH) lililofanyika katika viwanja vya Chuo cha Uhasibu Mbeya (TIA).


"Na niwasihi ndugu wananchi furaha unaitafuta wewe mwenyewe hayupo ambaye anaweza kukuletea furaha kwenye moyo wako jitahidi kuitafuta furaha ilipo ili uweze kubururudisha Moyo , hivyo furaha huwezi kuletewa na mtu mwingine na hata akikuletea ataleta kwa muda mfupi bali jitahidi uitafute  mimi niendelee kuwasisitiza ndugu zangu tufanye mazoezi mara kwa mara ili kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza "amesema Homera.


Aidha Homera amewataka wananchi mkoani hapa kuendelea kupima  afya zao mara kwa mara  kwani unaweza ukawa unatembea ukajiona mzima  ghafla ukaanguka na kupoteza maisha kwasababu hawana utamaduni  ,tuna hospitali nzuri kabisa na  Rais .Dkt.Samia Suluhu Hassan ameweza kuleta mashine nzuri za kisasa(MRI) badala ya kwenda Jijini Dar es Salaam na Dodoma hivi sasa huduma hizo zinapatikana Jijini Mbeya.



Mkurugenzi mtendaji wa Hospitali ya rufaa kanda ya Mbeya,Dkt.Godlove Mbwanji amesema kuwa kuwa wamekuwa wakishirikiana na jamii wanayohudumia kwa kufanya nao michezo pamoja na kuhamasisha watu kufanya mazoezi ili kuepukana magonjwa sugu yasiyoambukiza.


Dkt.Mbwanji amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan moja ya changamoto kubwa  ni magonjwa sugu yasiyoambukiza kuongozeka kwa kasi na yamekuwa yakiongeza gharama kubwa kwenye matibabu .


Amesema hivyo mkakati wa serikali ni lazima kubadilisha mfumo wa maisha kupenda mazoezi na namna ya ulaji wa vyakula pamoja na kupima afya ili kama mtu ana matatizo ili kama umegundulika uweze kutibiwa kirahisi.



Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi na Mkurugenzi wa Tiba katika hospitali ya Rufaa kanda ya Mbeya,Dkt.Uwesu  Mchepange amesema kuwa lengo kuu la bonanza hilo ni kuwakutanisha watumishi wa hospitali wakiwemo wastaafu pamoja na wananchi ili waweze wananchi waweze kutambua kazi zinazofanywa na hospitali ya rufaa kanda ya Mbeya.


Amesema kuwa bonanza hilo mpaka Sasa limefanyika mara ya Tisa ambapo lengo ni kuwakutanisha watumishi na wananchi katika mazingira tofauti na ya hospitali na kunakuwa na shughuli mbali mbali huwa zinafanyika kupitia tukio hilo ikiwemo upimaji wa afya bure ili wananchi waweze kutambua afya zao pamoja na kupata ushauri na shughuli zingine.



Sadock Sanane ni mtumishi wa Mahakama kuu amewataka wananchi kujenga mazoea ya kufanya mazoezi ili kuepuka kupata magonjwa yasiyoambukiza na kupunguza ulaji usiofaa.


Mwisho.

[11/5, 5:18 PM] Hamida Md Dom: Na Hamida Ramadhani, Matukio Daima App Dodoma


NAIBU Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira  Khamisi Hamza Khamisi ametaka fedha zitengwe ili kutatua changamoto kwenye uhifadhi wa Mazingira na mapambano dhidi ya mabadiliko na athari ya tabia nchi kwani ni janga la dunia


Haya ameyasema jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Ukusanyaji wa Mapato ya ndani kwenye sekta ya uzinduaji unavyoweza kufadhili mabadiliko ya tabia nchi ambapo Naibu Waziri huyo amesisitiza na nakuta fedha zinazokusanywa kwenye ripoti hiyo zijiekekeze kwenye kampeni za kitaifa za Mazingira kama vile  kampeni ya soma na mti.


Amesema fedha zitakapo patikana kwenye sekta ya Gesi, Nishati na Madini zielekezwe na ziendeleze kampeni za serikali zilizoanzishwa za kutunza mazingira na kukabiliana na mabadiko ya tabia nchi. 


" Nchini kwetu tatizo la uharibifu wa Mazingira lipo kwa kiasi kikubwa na hiyo yote nikutokana na uelewa mdogo kwa wananchi juu ya umuhimu wa utunzaji wa Mazingira  na ndio maana wanajikatia miti hovyo hawaliurimii taifa wao wanaamini ni jambo la kawaida ni wajibu hawakosei," Amesema. 


Na kuongeza " Ripoti hii iende ikatoe elimu katika jamii umuhimu wa kupanda na kutunza miti na Mazingira kwa ujumla tusipo fanya hivyo vizazi vijavyo vitakuja kujua kuwa asilimia kubwa ya Tanzania ni jangwa kumbe ni kutokana na ukataji wa miti, " Amesema Naibu Waziri Khamisi


Pia ameekeza ripoti hiyo ijikite kwenye Utunzaji wa vyanzo vya maji kwani bado kuna changamoto watu wanachepusha maji wanatoa maji katika asili yake na kupeleka mashambani kwao. 


Amesema watu wamesahau sheria ya Mita 60  wanalima karibu na mito wanatumia mbolea za sumu zinakwenda kwenye vyanzo vya maji na kupelekea viumbe hai wengine kufa au kupotea  kwenye Mito. 


" Sasa Ripoti hii iimize na kuzungumza juu ya utunzaji wa vyanzo vya maji kwani ukweli ni kwamba Mito ni maisha yetu, " Amesema. 


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Policy Forum Christina Ruhinda amesema wanachama wa Policy Forum wapo kwenye taasisi mbilimbali ambazo zinashughulikia masuala yanayohusu sekta zote hapa nchini. 


Amesema wanachama wanagusa mipango yote na kushikilia katika utekelezaji ili kuhakisha Tanzania inafikia maendeleo yaliojipangia kimkakati kuyafikia na kuchangia katika ukuaji na kuhakisha uwajibikaji na ufanyaji kazi kwa watu wote. 


Naye Makupa Nsendaluka  Afisa sera kodi na usimamizi wa rasilimali 

amesema kama ilivyo kwa nchi nyingi zinazoendelea, Tanzania imeathiriwa Sana na mabadiliko ya tabianchi madhara ambayo hayaishii tu kusababisha mafuriko na ukame lakini yanaharibu Miundombinu na hata kuathiri maisha ya watanzania. 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI