Header Ads Widget

OCEAN ROAD WAANZA RASMI UTOAJI WA HUDUMA ZA KIBINGWA ZA UCHUNGUZI NA UGUNDUZI WA SARATANI KAGERA


Na Matukio Daima App Bukoba

Madaktari bingwa kutoka Taasisi  ya Saratani  Ocean Raod  wameanza rasmi utoaji wa huduma za uchunguzi na ugunduzi wa saratani mkoani kagera.

Huduma hizo  zimeanza kutolewa rasmi leo Oktoba 31, 2023 hazi Novemba 02, 2023   katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba ambapo wananchi wamepata nafasi ya kupata huduma za kibingwa za uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi matiti na tezi dume.


Akitoa elimu kwa wananchi waliojitokeza kupata huduma hizo meneja wa  huduma ya kinga ya Saratani katika Taasisi hiyo Dr. Maguha Stephano amesema kuwa, wamefika Mkoani Kagera kutoa huduma ya uchunguzi wa Saratani kwa wananchi kwa lengo  la wakuwasogezea huduma hiyo karibu pamoja na kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kufanya vipimo vya ugonjwa wa saratani.


"Sisi kama Taasisi ya Ocean Road tumeona ni vyema kufika katika Hospitali za rufaa za mikoa   hususani maeneo ambayo ni mbali na Dar es  salaam  ambako Taasisi ipo ya huduma hizi za Saratani, pia niagizo  la Mhe Rais wetu Dr Samia Suluhu Hassani kwamba Hospitali za kibingwa ziwe zinakuja katika  Hospitali za rufaa za mikoa  ili kuweza kuwasaidia wananchi hasa hasa wale wakipato  cha chini ambao hawawezi kuzifikia Hospitali za kibingwa kupata huduma hizi,  kwahiyo tuko hapa  siku hizo tatu kwa ajili ya  kueleimisha umma na kufanya uchunguzi wa Saratani hizo"amesema Stephano.


Amefafanua kuwa ugonjwa wa Saratani umekuwa ukiongezeka  kutokana na sababu mbalimbali, takwimu za mwaka jana 2022 zinaonyesha kuwa, upande wa akina mama Saratani ambayo iliongoza kuwa na wagonjwa wengi ni Saratani ya mlango wa kizazi ikifuatiwa na Saratani ya matiti huku saratani ya koo la chakula  ikiongoza kwa upande wa wanaume ikifuatiwa na saratani ya tezi dume.


Aidha, ametaja dalili ya Saratani kuwa ni pamoja na  kuwa na  uvimbe unaotokea  sehemu husika ya mwili Saratani ilipo  ambapo ametole mfano wa Saratani ya titi inakuwa na dalili ya uvimbe sehemu ya titi, kwa pani, chuchu kubonyea ndani au  kutoa damu na maji maji meusi huku akiendelea kuwasisitiza wananchi wa Mkoa wa Kagera kuendelea kujitokea kufanya vipimo kwa siku zilizobaki.


Nao baadhi ya  wananchi waliojitokeza kupata huduma hiyo akiwemo  Jaysce Mgayuki na Sara Kamugisha wameishokuru Hospitali ya Rufaa ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba pamoja na madakta bingwa kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road kutoa huduma hizo bure.


"Tumekufurahishwa na ujio wa huduma hizi Mkoani Kagera kwani imewasaidia vyema kutambua hali ya afya zetu  dhidi ya Saratani naitatuwawezesha kupata matibabu kwa wale watakaokuwa wamebainika kuwa na dalili za ugonjwa huu  hivyo  niwaombe wananchi ambao bado hawajafika waendelee wamewasihi wananchi  kuendelea kujitokeza kwa kasi ili kupata  huduma hiyo muhimu muhimu zinazotolewa bure kabisa"

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI