Header Ads Widget

NGAYARINA AONYA UHARIBIFU WA MAZINGIRA MTO MALAGARASI

Michael Ngayarina Mkuu wa wilaya Buhigwe akiongoza zoezi la upandaji miti milioni mbili mpango unaosimamiwa na Program ya TUUNGANE kando ya mto Malagarasi uzinduzi uliofanyika kijiji cha Biharu wilaya ya Buhigwe
 


Na Fadhili Abdallah, Kigoma



Mkuu wa wilaya Buhigwe Michael Ngayarina amesema kuwa bonde la ziwa Tanganyika ukiwemo mto Malagarasi unadidimia kutokana na uharifu mkubwa wa mazingira hivyo amesema serikali itachukua hatua kali kwa watu wote watakaokamatwa wakihusika na uharibifu huo.




Ngayarina alisema hayo akizindua zoezi la upandaji miti kuzunguka mto Malagarasi ambapo kiasi cha miti milioni mbili inatarajiwa kupandwa.



Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa serikali itasimamia kwa karibu sheria na taratibu za mazingira na amewaonya watu wote wanaoharibu mazingira ukiwemo mpango potofu wa kuchoma mapori kwa kigezo cha kupima umri.

 


Pamoja na hilo Mkuu huyo wa wilaya  amewataka wadau wote  wakiwemo mwananchi wa kawaida kuona kuwa uhifadhi na utunzaji wa mazingira ni sehemu ya maisha yao ya kila siku.


Lukindo Hizza Mkurugenzi wa Program ya TUUNGANE  akishiriki zoezi la upandaji miti milioni mbili mpango unaosimamiwa na Program hiyo kando ya mto Malagarasi uzinduzi uliofanyika kijiji cha Biharu wilaya ya Buhigwe


Akizungumza katika mkutano huo Mkurugenzi wa Program ya TUUNGANE inayofadhiliwa na Shirika la The Nature Consevancy na Path Finder, Lukindo Hizza alisema kuwa shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo, ufugaji, ukataji mbao na shughuli nyingine nyingi  zimefanya eneo kubwa la bonde la Mto Malagarasi kuendelea kuathiriwa kwa maji yake kupungua na kubeba mchanga mwingi kupeleka ziwa Tanganyika.


Lukindo  alisema kuwa pamoja na mpango huo bado jitihada kubwa zinahitajika kutoa elimu kwa wananchi kuhusu uhifadhi na utunzaji wa mazingira wa bonde la Mto Malagarasi.




Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI