Home
About
Contact
Header Ads Widget
Home
News
Entertainment
Sports
Magazeti
Home
kitaifa
MJUKUU WA HAYATI MWALIMU JULIUS NYERERE ALIYEKUWA ANAISHI SHINYANGA KUZIKWA KESHO BUTIAMA MKOANI MARA
MJUKUU WA HAYATI MWALIMU JULIUS NYERERE ALIYEKUWA ANAISHI SHINYANGA KUZIKWA KESHO BUTIAMA MKOANI MARA
Misalaba
Monday, November 13, 2023
Mwenyekiti wa mtaa wa Mabambase Bwana Seif Nassor Hemed akizungumza.
Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Mwili wa Edward Majige Nyerere ambaye ni Mjukuu wa Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius kambarage Nyerere umesafirishwa leo kwenda Butiama Mkoani Mara kwa Mazishi.
Marehemu Edward Nyerere mwenye umri wa Miaka 26, alifariki dunia juzi siku ya jumamosi Novemba 11,Mwaka huu 2023 kwa ajali ya pikipiki aliyokuwa akiendesha,iliyotokea majira ya saa 12.00 asubuhi katika Barabara ya Uhuru eneo la Bushushu.
Edward Nyerere alikuwa mtumishi wa NIDA Mkoa wa Shinyanga ambaye alikuwa akiishi Mtaa wa Mabambasi kata ya Ndembezi katika Manispaa ya Shinyanga.
Akizungumza mwenyekiti wa mtaa wa Mabambase Bwana Seif Nassor Hemed ambaye ameelezea namna alivyopokea taarifa za tukiola kifo cha marehemu huyo.
Baadhi ya wakazi wa Mtaa wa Mabambasi kata ya Ndembezi wameomba watumiaji wa vyombo vya moto kuhakikisha wanazingatia sheria na kanuni za usalama barabara ikiwa ni pamoja na kuepuka mwendo kasi.
Mazishi ya Edward Nyerere yanatarajiwa kufanyika kesho Jumanne Novemba 14,2023 katika kijiji cha Butiama Mkoani Mara,mahali alipozaliwa.
Post a Comment
0 Comments
MAGAZETI
NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI
TV News
World News
UZA NUNUA NASI LEO
Subscribe Us
MATANGAZO
TIBA YA UKANDAJI WA MGONGO, KICHWA KUTOKA NEEMA BEAUTY, SPA SALOON
MAKALA NZURI ZAIDI
TMDA YAUNGANISHA TANCIS NA RIMS, SASA WAINGIZAJI WA MIZIGO MIKUBWA YA FORODHA KUTUMIA MFUMO WA TANCIS
Andrew Chale
Thursday, April 09, 2026
Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Dk. Adam Fimbo MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imewatan…
STAY CONNECTED WITH US
Ad Space
Responsive Advertisement
Most Popular
MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2025/2026
Saturday, January 31, 2026
AMBONI ADVENTURE RUN, FURSA YA KUTANGAZA MAPANGO YA AMBONI TANGA
Saturday, January 31, 2026
RAIS DKT.MWINYI ASISITIZA UMOJA,MAADILI NA MALEZI BORA YA VIJANA
Saturday, January 31, 2026
Contact form
0 Comments