Header Ads Widget

CCM TANGA WAONYA WATENDAJI WAZEMBE

Na Mbaruku Yusuph Matukio Daima APP Tanga. 

CHAMA cha Mapinduzi(CCM) Mkoani Tanga kimesema hakitakubali kuona wananchi wanataabika wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatoa fedha kwa ajili ya kuondoa changamoto zinazowakabili.


Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa chama hicho Mkoani hapa Rajabu Abdurahman wakati wa ziara yake ya kawaida ambapo aliambatana na kamati ya Siasa Mkoa na Wilaya iliyokuwa na lengo la kuangalia malalamiko ya wananchi na kukagua miradi ya Serikali.


Rajabu alisema Serikali imetenga fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo na ile ya kijamii jambo la kushangaza wapo baadhi ya viongozi wa Serikali wanazikalia fedha hizo badala ya kutumika ipasavyo kama ilivyokusudiwa.

"Salamu ziwafikie wote waliopewa dhamana na Serikali ndani ya Mkoa wa Tanga wajue wanalojukumu la kutimiza wajibu wao na si vinginevyo"Alisema Abdurahman. 


Aidha alisema ziara zake hizo za mara kwa mara ndio tafsiri sahihi ya kukitendea haki Chama na Serikali kwa ujumla na watendaji wa Serikali watambue kuhojiwa kwao juu ya utekelezaji wa miradi ya Serikali si jambo baya kwao bali ni namna gani ya Chama kinavyotaka kujiridhisha na utendaji wao.


"Lakini watumishi hao wa Serikali wajue hatuwezi kukubali kuwaona wananchi wenzetu wakitaabika na kusulubika wakati Serikali kupitia Rais Samia Suluhu Hassan anatoa pesa kwa ajili ya kuwaondolea changamoto zinazowakabili wananchi lakini jambo la kusikitika pesa zinatumwa na viongozi wamezikalia na niliwa hikusema katika mkoa wa Tanga ni mwisho"Alisema Abdurahman. 

Hata hivyo alitumia ziara hiyo kuwaomba viongozi wa ccm kwa nafasi zote za chama Mkoani Tanga na jumuiya zake watambue  changamoto zinazowakabili wananchi zisisubiri viongozi wakuu wa Serikali na Chama waje na wananchi walalamike kwa vingozi hao kitendo hicho hakileti afya.


Mwenyekiti huyo pamoja na kamati yake ya siasa alitembelea katika mradi wa vyoo katika shule ya sekondari ya Mnyanjani,barabara ya masiwani na bustani ya Forodhani ambapo kunajengwa mradi wa eneo la mapumziko.


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tanga James Kaji alisema wapo mafundi kichefuchefu ambao wamekuwa wakichukua kazi nyingi huku wakikosa uwezo wa kuisimamia na kusababisha kutokukamilisha miradi.


Aidha alisema zipo dalili zinazoonyesha mafundi hao wanawatumia baadhi ya watendaji kwa sababu ya kutoa rushwa ili wafanikishe kupata kazi hizo au kuwa na mahusiano ya kiundugu au  urafiki nao.


"Wapo mafundi ambao haoni sababu ya kufanya kazi katika Wilaya yangu kutokana na kutokuwa na uwaminifu mzuri 

Utamkuta fundi baada ya malipo ya awali anakimbia eneo la kazi  hizi ndio shida ya mafundi wetu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI