Header Ads Widget

WANAFUNZI WACHUANA UBUNIFU WA KISAYANSI LINDI

 


NA HADIJA OMARY,LINDI

TAASISI ya wanasansi chipukizi Tanzania (YST) imendesha mashindano kwa wanafuzi wanaosoma masomo ya sayansi katika shule 15 Mkoani Lindi yenye lengo la kuwajengea uwezo wanafunzi  wa kitaalam wa kubuni tafiti za kisayansi zenye kuleta tija kwa jamii.

 

Hatua hiyo inakuja kufuatia kuwapo kwa mwamko mdogo wa wanafunzi katika kuyapenda masomo ya sayansi hapa nchini ambapo inaelezwa mpango huo wa kuwajengea uwezo wanafunzi katika masomo ya sayansi umekua ukitekelezwa toka mwaka 2011 na Tasisi ya wanasayansi chipukizi hadi sasa umeonekana kuanza kuleta matunda.

 


Akifunga mashindano ya wanafunzi walioshiriki bunifu za kisayansi yaliyofanyika kataika shule ya secondary WAMMA Sharaf Mkoani Lindi Afisa elimu mkoa huo Mwl Joseph mabeyo  akatumia fursa hiyo kuwakumbusha walimu kutunza takwimu za ubunifu huo ili watalaam hao tarajali wasipotee.

 

Awali mwanzilishi mwenza wa Taasisi ya Wanasayansi Chipukizi Young Scientists Tanzania  (YST), Dk Gozibert Kamugisha amesema Wanafunzi hao wamekutanishwa kupitia mpango wa kuwajengea uwezo na ujuzi wanafunzi wa Sekondari kwenye masomo ya sayansi nchini unaotekelezwa na YST chini ya ufadhiri wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee Foundation na kampuni ya Kimataifa ya nishati shell Tanzania.

 

Dk Kamugisha ameongeza kuwa  uwepo wa mashindano kwa wanasayansi chipukizi kumesaidia kuongeza ari na kukuza bunifu mbalimbali za kisayansi ambazo wanafunzi wamezibuni na kuwa na msaada mkubwa kwao na katika jamii zao.

 

 

Kwa upande wake Mshauri Mkuu wa masuala ya Kijamii kutoka kampuni ya shell Tanzania Msomisi Mbenna ameeleza kuwa tangu mwaka 2013 wamefadhiri Mradi huo ili kuboresha sayansi katika shule za sekondari jambo linalosaidia kuwa wabunifu na kuwa watafiti huku Afisa elimu wa Mkoa wa Lindi Joseph Mabeyo aliyekuwa mgeni rasmi katika halfa hiyo ameendelea kuwatia moyo wanafunzi kuendelea kusoma masomo hayo kwani bado nchi inahitaji kuweza kulisaidia Taifa.

 

Daniel Mlelwa na Janerose Augustin ni wanafunzi wa Nkowe sekondari  kutoka wilaya ya Ruangwa ambayo  ilibuka kinara kupitia ubunifu wa kutengeneza dawa ya tumbo na kuzuia kuhalisha kwa kutumia magome ya mwembe  wamesema uwepo wa mashindano kama hayo yanawasaidia tafiti na gunduzi  zao kuenda juu zaidi ambapo wanaamini watafanikiwa kufikia ndoto zao.

 

Kukamilika kwa mashindano ya maonyesho ya sayansi kwa wanafunzi ni maandalizi ya kuelekea mashindano ya kitaifa hapo disemba 7 mwaka huu ambapo mshindi wa 1 na 2 kutoka mkoa lindi wanategemewa kushiriki katika michuano ya kitaifa.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI