Mwenyekiti wa wajasiliamali eneo la viwanda vidogo (SIDO) Manispaa ya Kigoma Ujijiji Hamisi Abdallah
Na Fadhili Abdallah, Kigoma
WAJASILIAMALI wanaofanya shughuli zao katika eneo la viwanda vidogo SIDO manispaa ya Kigoma Ujiji wamepinga viwango vikubwa vya kodi ya pango vilivyowekwa na shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) wakitaka viwango hivyo vipunguzwe.
Wakizungumza na waandishi wa habari katika mkutano walioitisha ili kujadili suala hilo wajasilimali hao walisema kuwa viwango vilivyowekwa ambavyo ni ongzeko la zaidi ya asilimia 100 ni vikubwa lakini wajasilimali hao hawakushirikishwa katika upangaji wa bei hizo mpya.
Mwenyekiti wa wajasiliamali katika eneo hilo, Hamisi Abdallah alisema kuwa wanashangazwa kuona SIDO inatangaza viwango vipya vya kodi ya pango bila kukaa na wajasiliamali kuzungumza kwa pamoja kuona uhalisia wa viwango hivyo na hali ya biashara kwa sasa hivyo hawatakubali kulipa viwango vipya kama hawatakaa na kuzungumza.
Baadhi ya wajasiliamali waliokuwepo kwenye mkutano huo Joseph Nyurahe maarufu Chinga na Mwalim Ngereza Kishumbu walisema kuwa viwango vya kodi ya pango vlivyowekwa na SIDO na vikubwa na havikuwa shirikishi hivyo hawakubaliani navyo.
Gervas Ntahamba Meneja wa SIDO Mkoa Kigoma
Akizungumzia sakata hilo Meneja wa SIDO mkoa Kigoma, Gervas Ntahamba amethibitisha kupanda kwa bei ya kodi ya pango kwa vibanda vilivyopo eneo la viwanda SIDO mkoa Kigoma na vimeanza kutumika rasmi mwezi Julai mwaka huu.
Ntahamba alisema kuwa viwango hivyo vimewekwa na uongozi wa SIDO makao makuu kupitia vikao vya bodi na maelekezo hayo yametolewa kwa SIDO nchi nzima na viwango hivyo vinakuja kufuatia tathmini iliyofanywa hivyo vimepangwa kulingana na bei ya soko ilivyo sasa kulingana na kila eneo
0 Comments