Na,Jusline Marco:Arumeru
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Arusha Sulemani Msumi amewataka wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Mwandeti kuzingatia kanuni ya 6K kwenye ufanyaji wa mitihani yao ya kuhitimu elimu ya sekondari wanayoitarajia kuifanya Novemba 13 mwaka huu.
Msumi ameyasema hayo kwenye maafali ya 17 ya kidato cha nne katika shule hiyo na kusema kuwa kufaulu kwa kiwango cha juu kunatokana na kanuni hiyo ambayo ni kuzingatia muda,kusoma kwa bidii,kupumzika,kunywa maji,kujiamini pamoja na kuomba Mungu.
Aidha amewataka walimu katika shule hiyo kuongeza juhudi kuhakikisha vijana hao kuendelea kuioeperusha vizuri bendera ya halmashauri ya Arusha kwa kuendelea kung'ara kimatokeo.
Akijibu baadhi ya changamoto zilizowasilishwa katika risala ya mkuu wa shule hiyo ikiwemo uhaba wa vitabu, Msumi amesema kuwa halmashauri ya Arusha imepokea jumla ya vitabu 27900 mbapo jumla ya vitabu 1400 vimetolewa katika shule hiyo.
Ameongeza kuwa suala la changamoto ya uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi nila kisera kwani walimu ambao wamekuwa wakipewa hawatoshelezi shule za sekondati 35 zilizopo katika halmashauri ya Arusha, ameutaka uongozi wa shule hiyo kuendelea kutumia mfumo wa walimu wanaojitolea ili kueza kutoa elimu kwa wanafunzi badala ya kukaa na kusubiria mgao wa walimu kutoka serikali kuu.
Awali katika risala yake mkuu wa shule ya Mwandeti Mwl.John Massawe amesema kuwa kufuayi mtihani ya upimaji ya KPI uongozi wa shule hiuo umebaini kuwepo kw wanafunzi wasiomudu somo la kingereza ambapo pia amesema kama shule wanakabiliwa na upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi.
Pamoja na shule hiyo kuwa na idadi ya wanafunzi 1726,wavulana wakiwa 693 na wasichana 1033 kati ya hao wanafunzi 329 wanatarajiwa kuanza mitihani yao ya kuhitimu elimu ya sekondari Novemba 13 mwaka huu ambapo shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri kitaaluma mwaka hadi mwaka na kushika nafasi ya kwanza kimkoa kwa watahiniwa chini ya 30.
0 Comments