Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP Njombe
Mashindano ya Mpete Diwani Cup kwa wanafunzi wa shule za msingi kata ya Utalingolo wilayani Njombe yametamatika kwa timu ya mpira wa miguu Utalingolo kuibuka mshindi dhidi ya timu ya Nole fc baada Ya mvutano mkali uliwafikisha hatua ya mikwaju ya penati.
Baada ya mchezo huo makepteni wa timu zilizofika fainali Boneventura Mwalongo kepteni timu ya Utalingolo na Deus Myamba kepteni timu ya Nole wakaeleza namna walivyoshiriki tangu mashindano yalipoanza na kwamba kujituma katika mazoezi na kuwasikiliza walimu ndicho kilichowafikisha hatua ya fainali.
Muandaaji wa mashindano hayo Diwani wa kata ya Utalingolo ambaye pia ni mwenyekiti wa halmashauri Ya mji wa Njombe Erasto Mpete amesema ameona ni muhimu kuandaa mashindano hayo ili kuibua vipaji vya watoto badala ya kuendelea na mashindano ya vijana pekee.
Mgeni wa heshima katika fainali hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Ruhuji kijiji cha Utalingolo ofisa elimu msingi Halmashauri ya mji Njombe Mwalimu Shida Kiaramba awali akifungua mashindano hayo ambayo yalikua na michezo ya mpira wa miguu na Netball kwa wasichana amesema anataka kuona mashindano hayo yanakwenda katika kata zote badala ya kuchezwa kwenye kata moja pekee.










0 Comments