Header Ads Widget

UN YAUNGA MKONO CHAKULA MASHULENI

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

MASHIRIKA 16 ya Umoja wa Mataifa yanayofanya shughuli zake mkoaji Kigoma umesema kuwa kutolewa yanaunga mkono mpango wa serikali wa kutoa  chakula shuleni kutokana  uhusiano makubwa uliopo  wa wanafunzi wanaopata chakula shuleni kufanya vizuri  kwenye masomo yao hivyo imetangaza kuendelea kuunga mkono serikali kufanikisha mpango huo.

Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa mkoani Kigoma,Kanali Ranko alisema hayo akitoa salamu mbele ya Naibu Waziri wa kilimo na mifugo, Alexender Mnyeti alitembelea kituo cha wanafunzi maalum Bitale mkoani Kigoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya chakula duniani ambayo kitaifa inafanyika mkoani Kigoma.


Mratibu wa mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa mkoani Kigoma Kanali Ranko (kulia aliyesimama) akizungumza wakati Naibu waziri wa mifugo na Uvuvi Alexander Mnyeti alipotembelea shule ya msingi Maalum Bitale ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya chakula duniani


Ranko alisema kuwa tafiti zinaonyesha kuwa wanafunzi ambao hawapati chakula wamekuwa wakipata taabu kuzingatia masomo lakini pia wanafunzi ambao wamekuwa wakipata chakula kinachozingatia aina mbalimbali za chakula bora ufaulu wao umekuwa mkubwa wanapozingatia masomo.

Kutokana na hilo alisema kuwa mpango huo ni mzuri na kwamba Umoja wa Mataifa kupitia mpango wa pamoja Kigoma unaosimamiwa na mashirika 16 ya Umoja wa Matifa wataendela kuunga mkono mpango huo ambapo walikabidhi treni 100 za mayai kwa uongozi wa shule maalum Bitale kuchangia vyakula vya protini na vitamin kwa wanafunzi wa shule hiyo.

Akizungumza shuleni hapo Naibu Waziri wa mifugo na uvuvi, Alexander Mnyeti  aliwakumbusha viongozi wakiwemo wakuu wa mikoa hadi serikali za mitaa, vijiji na wazazi kuzingatia kutoa chakula kinachozingatia lishe bora ili kupunguza udumavu kwa watoto.

Mnyeti alisema kuwa inashangaza kuona mkoa Kigoma unauzalishaji mkubwa wa mazao mbalimbali ya chakula, samaki na dagaa na vyakula vingine hivyo haiingii akilini kuona wazazi wanawalisha watoto mihogo na mahindi pekee ambavyo havina protini wakati vipo vyakula vingine ambavyo wanaweza kuvitumia na watoto wao kuwa na afya bora.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI