WANAHISA wa Kampuni ya TCCIA Investment wametakiwa kuhakiki taarifa zao ili waweze kulipwa gawio lao ambalo limefikia kiasi cha shilingi milioni 350.
Akizungumza Mjini Kibaha wakati wa kikao na wanahisa hao ofisa mtendaji mkuu wa kampuni hiyo Peter Kifungomali amesema fedha hizo bado hazijagawiwa kutokana na sababu mbalimbali.
Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa chemba ya wafanyabiashara ya TCCIA Mkoa wa Pwani Fadhili Gonzi amesema kuwa baadhi ya wanahisa walikuwa na maswali mengi juu ya fedha zao.
Naye mmoja wa wanahisa Ayubu Mtawazo amesema kuwa hisa ni moja ya sehemu salama ya kuwekeza fedha ambapo watu wengi wamenufaika.
Clara Ibihya amesema kuwa manufaa ya hisa ni makubwa kwani ukishawekeza fedha zako hupati tena usumbufu kutakiwa marejesho bali unasubiri kupata fedha.
0 Comments