Header Ads Widget

SHAMBA LA MBEGU KILIMI NZEGA KUONGEZA UZALISHAJI WA MBEGU KUTOKA TANI 200 HADI TANI 3000 KWA MWAKA

 


Na Lucas Raphael,Tabora

 

SHAMBA LA MBEGU KILIMI NZEGA KUONGEZA UZALISHAJI WA MBEGU KUTOKA TANI 200 HADI TANI 3000 KWA MWAKA   

 

Serikali imetakiwa kuendelea kulisaidia Shamba la Mbegu kilimi wilayani Nzega kuendelea kutumia  teknolojia ya umwagiliaji ambayo ndio  suluhisho pekee la kuchochea mapinduzi ya kiuchumi kwa kuongeza uzalishaji wa mbegu kutoka tani 200 hadi tani 3000 kwa mwaka .

 

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyetikiti wa kamati ya ya kudumu ya bunge ya Viwanda Biashara Kilimo na Mifugo Mariam Ditopile mara baada ya  kushuhudia uwekezaji mkubwa unaotekelezwa na serikali katika  mradi wa umwagiliaji kwenye  shamba la Kilimi kuzalisha Mbegu bora za kilimo lililopo wilayani Nzega mkoani Tabora

 

Alisema kuwa teknolojia ya umwagiliaji ndiyo njia pekee itakayoleta mapinduzi ya kiuchumi na kijamii hapa nchini kupitia sekta ya kilimo .

 

 


 

Mariam alisema kwamba serikali iendelea kuwekeza maeneo mengine kwa ajili ya upatikanaji wa mbegu bora za kilimo jambo ambalo litafanya bei ya mbegu kupungua tofauti na ilivyo sasa .

 

 Alisema kwamba wizara ya kilimo iombe fedha kiasi chochote wanachotaka kwenye bajeti kuu ya serikali kwa ajili ya kuendelea na kuboresha teknolojia ya umwagiliaji .

“Kamati ya bunge kauli mmoja tunapongeza kazi nzuri unayofanywa na wakala wa mbegu nchini Asa kupitia mtendaji mkuu wa ASA kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kuhakikisha fedha zilizitolewa na serikali zinafanya utekelezaji uliobora na wenye tija” alisema Ditopile.

Alisema kwamba kupitia teknolojia ya umwagiliaji  uzalishaji wa  mbegu utaongezeka kutoka tani 200 kwa mwaka 2022 hadi kufikia tani 3000 kwa mwaka 2024 utasaidia kupunguza kiasi kikubwa cha mahitaji ya mbegu nchini .




Awali Naibu Waziri wa Kilimo Davidi Silinde aliambaia kamati hiyo kwamba serikali inaendelea na jitiada za kuboresha mashamba ya wakala wa mbegu kwa kuwapatia fedha na kwa ajili ya utekelezaji wa teknolojia ya umwagiliaji ili kuweza kuzalisha mbegu kwa kipindi chote cha mwaka .

Alisema kwamba lengo la serikali ni kuhakikisha nchi inazalisha mbegu nyingi na hilo linasababishwa na kuangiza mbegu kutoka nje ya nchi kwani fedha nyingine za kigeni zinatumika kwa kazi hiyo .

Ndoto ya mheshimwa Rais ni kutumia mashamba yetu kupitia kwa wakala wa mbegu nchi ambao ni ASA kuzalisha mbegu bora na mfano mzuri ndio hapa kilimi ambapo utaona teknolojia ya umwagiliaji inafanya kazi ya uzalishaji wa mbegu“alisema Naibu wa waziri Silinde

Hata hivyo alisisitiza kwamba kazi ya kuzalisha mbegu sio serikali pekee yake itafanya kuwaalika watu na Sekta binafsi kuja kuja kuungana nasi.

Nainu waziri aliwatoa hofu wadau wazalishaji wa mbegu kujitokeza kupata elimu na maelekezo  ili kuungana kwa pamoja kwa ajili ya kuzalisha mbegu zilizokuwa bora za kilimo,

Shamba la mbegu la Kilimi uzalisha mbegu za Alizeti, Choroko ,Mahindi na Mtama  na kuzisambaza katika ukanda wa magharibi na ziwa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI