NA CHAUSIKU SAID
MATUKIO DAIMAAPP MWANZA.
Mrajis wa vyama vya ushirika Benson Ndiege amezitaka SACCOS zote ambazo zinaendesha Shughuli za matawi na milango ya huduma zikiwa hazijaomba leseni kusitisha biashara zao mara moja mpaka pale zitakapoomba leseni.
Kauli hiyo ameitoa jijini Mwanza katika kilele Cha maadhimisho ya ushirika wa akiba na mikopo na kueleza kuwa ni kosa la jina kuendesha Shughuli kinyume na seria na taratibu zilizowekwa.
Ndiege amesema kuwa Saccos zote zenye matawi na milango ya huduma zinapaswa kuhakikisha zinatekeleza matakwa ya sheria na kuepukana na adhabu zinazoweza kutozwa pamoja na hatua zinazoweza kuchukuliwa na ofisi dhidi yao.
"Nimesikia zipo baadhi ya SACCOS kama URA, KIFANYA, SAME KAYA na nyinginezo ambazo zina matawi Hadi sasa hazijaomba idhini ya kuendesha matawi hayo" Alisema Benson
Hata hivyo amefafanua kuwa tume ya maendeleo ya ushirika Tanzania inaendelea kuweka mikakati mbalimbali ya kuboresha utendaji kazi wa vyama vya ushirika Nchini ikiwemo SACCOS Kwa kuandaa vikao mbalimbali vya wadau Kwa lengo la kupeana taarifa.
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Elikana Balandya ambaye alikuwa mgeni rasmi Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Amos Makalla amevitaka vyama vya ushirika akiba na mikopo kuendelea kusimamia vyema rasimali Kwa kutambua Mfumo wa ushirika umeundwa mahususi kuhakikisha Kila mwanachama anashiriki kikamilifu katika kusaidiana.
Balandya amesema kuwa vyama hivyo ni lazima kuwa pamoja katika ushirika ambao utawasaidia kutambua kuwa wanaweza kutatua changamoto zinazowakabili, hivyo ili rasimali ziweze kuwanufaisha wanachama walio wengi lazima kuimalisha huduma Kwa kuongeza udhibiti wa ndani, masharti, kuboresha sera pamoja na kuzingatia sheria na taratibu za zote zilipo.
" pale tu tunapozingatia sheria na taratibu tulizojiwekea itatusaidia sana kuhakikisha tunaenda katika mwenendo ambao ni mzuri pia ningependa kuona ushirika unaendelea kuwa huru na ambao unajisimamia wenyewe Amesema Balandya.
Mjumbe wa bodi ya shirikisho la vyama vya ushirika Tanzania (TFC) Kolimba Tawa amesema kuwa Saccos ndio zinawajibu wa kuhakikisha Shirikisho la vyama vya akiba na mikopo (SCCULT) inasimama imara Kwa kuimarisha Mali za wanachama pamoja na kujitoa Kwa ajili ya chama.
"Bila saccos kuifanya sccult kusimama imara haiwezi kuwa imara changamoto zipo sehemu mbalimbali hapa duaniani hata kwenye familia zipo na vyama changamoto lazima ziwepo na ndio zitakazofanya kuendelea mbele, tuzifanyie kazi hizo changamoto ili Sccult iweze kuendelea mbele, amesema Kolimba.
0 Comments