Na Scolastica Msewa, Rufiji.
Mkuu wa mkoa wa Pwani Mheshimiwa Abubakari Kunenge amefika kutembelea Maeneo yenye viashiria vya kutokea athari za Mvua za Elnino huko Muhoro Rufiji mkoani Pwani ambapo amewataka kuhama maeneo hayo ili wasije kupatwa na athari za mvua za elinino zinzotarajiwa kunyesha.
Mheshimiwa Kunenge awali alitembelea kwa lengo la kukagua baadhi ya maeneo ya Kata ya Muhoro ambapo amefanya ziara hiyo wilayani Rufiji Tarafa ya Muhoro akiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele.
Aidha Mheshimiwa Kunenge alipata kuzungumza na wananchi wa Muhoro ambapo amewaasa kuzingatia maelekezo ya serikali ya kuhama eneo hilo ikiwa ni taadhari za kujihami na mvua hizo.
Mwaka 2021 eneo hilo liliathirika na Mvua kubwa na Serikali iliwatafutia eneo mbadala wananchi na kuwagawia viwanja.
Wananchi wamepongezwa na Serikali kwa uamuzi wao na kukubali kuhama.
0 Comments