Waziri wa Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo ametoa rai kwa Taasisi za Umma kuhakikisha zinafungamanisha  Sera na  Mipango ya taasisi hizo na Mipango ya Taifa  ili  kuwa na matumizi yenye tija kwa Rasilimali za nchi.
Prof. Mkumbo ameyasema hayo Octoba 4, 2023 mkoani Dodoma katika kikao kilichowakutanisha na Waziri wa Madini Mhe. Antony Mavunde kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa utekelezaji wa majukumu kati ya Ofisi ya Rais  Mipango na Uwekezaji na Wizara ya Madini.
Katika kikao hicho Mawaziri hao wamejifunza na kubaini Mipango ya Maenendeo na fursa za uwekezaji katika sekta ya madini ili kuzitangaza   duniani.
Kwa upande wake, Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amesema  Wizara yake imepanga  hadi kufika mwaka 2030 iwe imefanya utafiti wa kina wa kijiologia na jiofizikia kwa ajili ya kupata taarifa ya miamba na  madini  kufikia asilimia 50 ambapo kwa sasa ni asilimia 16 tu iliyofanyiwa utafiti wa maeneo yenye madini nchini.
Waziri Mavunde ameongeza kuwa uchumi wa madini unaonekana  kwa sasa  unatokana na asilimia 16 ya eneo lililofanyiwa utafiti wa kina akitolea mfano katika mwaka wa fedha 2022/2023 sekta ya madini imeongoza kwa mauzo ya  bidhaa za nje kwa asilimia 56 ambapo mauzo yamefanyika kwa zaidi ya Dola za Marekani bilioni 3.3.
Aidha, sekta hiyo ya madini imechangia katika kodi  ya mapato ya ndani  kwa asilimia 15 ambayo ni  zaidi ya trilioni 2 za  kitanzania.
Vilevile, Mavunde ameongeza  kuwa taarifa zitakazopatikana kupitia tafiti hizo  hususan tafiti za  miamba zitasaidia Wizara ya maji kufahamu maeneo yanayofaa kuchimba visima  vya maji na pia tafiti hizo zitasaidia Wizara ya kilimo kwa ajili ya uchimbaji wa mabwawa na kilimo cha umwagiliaji ili watanzania waepukane na kilimo cha kutegemea mvua.
Waziri Mavunde, alisisitiza tafiti zinazoendelea kufanyika  zitasaidia wachimbaji wadogo kufahamu maeneo yenye madini na kuondokana na adha ya kupata hasara kutokana na hali ya sasa ilivyo ya wachimbaji wengi kukisia maeneo ya uchimbaji. Pia, tafiti hizi zitaondoa  migogoro kati ya wachimbaji wakubwa na wadogo kwa kuwa uchimbaji utafanyika kwa katika maeneo yaliyofanyiwa tafiti..jpeg)
.jpeg)



.jpeg)





 
 
 
 
 
 
 
 
.jpg) 
0 Comments