Header Ads Widget

PAUL MAKONDA KAA KWA KUTULIA -

Nimesikia kauli ya ajabu kutoka kwa Katibu wa NEC itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda leo Oktoba 26, 2023.


Makonda amesikika akisema kuanzia leo Tanzania hakuna upinzani.


Nataka atambue kuwa tangu kuanza kwa Mfumo wa vyama vingi nchini 1992 hadi leo CCM ipo na vyama vya upinzani vipo na vimeimarika zaidi.  


Makonda ajue kuna viongozi ndani ya CCM waliomtangulia  na kuondoka kwenye hiyo nafasi upinzani wameukuta na wameuacha unashamiri kila kukicha huku CCM ikizidi kuporomoka. Kwa hiyo yeye hana jipya wala mwarobaini wa kuisaidia CCM.


Tunaishangaa zaidi CCM inayojidai ina wanachama wasomi mamilioni, leo imekosa mtu sahihi wa  kukisema chama na kumpa  Paul Makonda!


Makonda hana jipya zaidi ya ukatili huko alikotoka kwenye nafasi za Serikali hakuacha alama njema ya kukumbukwa na kutukuzwa, ameacha alama ya maumivu.


Hivyo CCM isitarajie alama njema kwa Makonda. Hana jeuri ya kuua upinzani,  zaidi ajiandae kuiua CCM.


JANETH JOEL RITHE 

N/NAIBU KATIBU MWENEZI 

ACT WAZALENDO

26/10/2023

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI