NA CHAUSIKU SAIDMATUKIO DAIMAAPP MWANZA
Jeshi la polisi Mkoani Mwanza limefanikiwa kukamata nyavu 815 za kuvulia samaki zinazozaniwa kuwa za wizi baada ya wavuvi walikuwa wakizitumia kuvulia kuzikimbia.
Akithibitisha kukamatwa Kwa nyavu hizo kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa Wilbroad Mtafungwa amesema kuwa wavuvi hao walikimbia baada ya askari wa kikosi Cha opareshioni kufanya msako wa kukamata watu wanaojihusisha na wizi ndani ya ziwa Victoria.
Mtafungwa amesema kuwa operashioni hiyo imekuja baada ya uwepo wa vitendo vya uhalifu Kwa baadhi ya wavuvi wasio kuwa wawminifu wanaotaka kupata faida Kwa haraka na kuwa tabia ya kuwapora wenzao samaki na kuwaibia nyavu pamoja na mashine za boti.
Kupitia opareshioni hiyo wameweza kuvifikia visiwa zaidi ya tano (5) vilivyopo ziwa Victoria vilivyopo upande wa Ukerewe, Nyamagana, Ilemela, Sengerema pamoja Mialo sita.
Hata hivyo ameeleza kuwa kupitia opareshioni hiyo wameweza kukamata injini za boti 12 pamoja na mitumbwi 22 huku mitumbwi 18 imekutwa na nyavu 387 zikiwa zimeibiwa kutoka sehemu mbalimbali kutoka Kwa wavuvi wanaovua ziwa Victoria.
"Baada ya kukamata nyavu hizo zimeweza kutambuliwa na baadhi ya watu waliokuwa wamekuja kushitaki katika vituo vya polisi kuwa wameibiwa nyavu zao" Alisema Mtafungwa.
Mitumbwi mingine minne iliyosalia ilikutwa haina usajili na ndani yake kuwa na nyavu haramu 10 ambazo haziruhusiwi kuvua samaki katika ziwa Victoria kutokana na kuvua samaki wadogo ambao hawajafikia kuvuliwa.
Aidha ametoa wito Kwa wavuvi wote wanaovua ziwa Victoria kuendelea kutoa taarifa na kujiepusha na kujihusisha na matukio ya kialifu
0 Comments