Header Ads Widget

MKURUGENZI MTENDAJI WA AKIBA COMMERCIAL BANK PLC AZINDUA RASMI WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

 


Na Mwandishi wetu


Benki ya Akiba PLC imewashukuru wateja wake kuichagua kwa kuendelea kuiamini katika kutumia huduma zake ikiwemo kuhifadhi ,kutuma na kutoa fedha huku wakiomba mikopo kwa ajili ya shughuli za kiuchumi.


Shukrani hizo zimetolewa leo Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Akiba Bw  Silvest Arumasi wakati  akizindua rasmi wiki ya huduma kwa wateja katika tawi la Kijitonyama ambapo amesema benki hiyo imekuwa ikitoa huduma nzuri kwa wateja wake na wikii hii inayofuraha kuwa pamoja na wateja wake tangu kuanzishwa kwakwe na .


 Katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Nawashukuru wateja kwa kuichagua na kuiamini Benki ya Akiba katika kuwahudumia nawaahidi  na kuwahakikishia wateja huduma bora  kutoka ACB hivyo Sherehe za huduma kwa wateja zina adhimishwa katika matawi yote ya ACB " amesema Bw: Arumasi 


Aidha  wateja wote wanaalikwa  kutembelea matawi ya Akiba kwa ajili ya kusherekea wiki hii ya huduma kwa wateja pamoja na kupata taarifa mbali mbali za huduma mpya na maboresho mbalimbali.

Pia  Mkurugenzi amewashukuru wateja wote walioshiriki katika zoezi la utafiti wa viwango vya uridhikaji katika utoa huduma yaani (Customer Satisfaction Survey) lililoratibiwa na kampuni huru ya kujitegemea kwa lengo la kuhakikisha uwazi na uhuru wa kutoa maoni kwa wateja.


 ACB inayoutamaduni wa kufanya utafiti huo  kila mwaka na hivyo amewasihi wateja kushiriki tena kikamilifu kwa lengo la kupata maoni na mirejesho itakayosaidioa kuboresha huduma zitolewazo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI