Header Ads Widget

MBUNGE DKT KIMEI AMSHUKURU RAIS DKT SAMIA SULUHU HASANI KWA MITUNGI YA GESI JIMBO LA VUNJO.



Na WILLIUM PAUL, MOSHI.

Mbunge wa Jimbo la Vunjo Dkt Charles Stephen amekabidhi mitungi 100 ya gesi kwa makundi mbalimbali wakiwemo wajasiriamali, mama lishe, baba lishe, wazee na baadhi ya shule za msingi na sekondari kama sehemu ya uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi na salama kwa afya na mazingira.



Dkt Kimei amesema ugawaji wa mitungi hiyo ya gesi bure kwa walengwa hao ni utekelezaji wa mpango kabambe wa kuhamasisha matumizi ya gesi asilia kwa wananchi ambayo ni safi, nafuu na salama unaotekelezwa na serikali ya CCM Awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.



"Tunamshukuru Rais wetu mpendwa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa mitungi hii ya gesi kwani ameonesha kwa vitendo kuthamini utunzaji wa mazingira na kuwajali wananchi tutaendelea kumuunga mkono kwa kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi." Alisema Dkt Kimei



Baadhi ya waliopokea mitungi hiyo akiwemo Peter Mnenei na Neema Kimati walisema kwamba kitendo cha kuwezeshwa mitungi hiyo ya Gesi kwao kitawasaidia kuwakomboa kiuchumi kwa sababu wanapokuwa kwenye shughuli zao watakuwa wakitumia muda mchache kuandaa na kuwahuduma wateja na wapendwa wao hivyo wanamshukuru sana Mbunge wao Dkt Charles Stephen Kimei kwa kuwajumuisha katika mpango huo.

Mwisho..

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI