Header Ads Widget

MAONYESHO YA DAR CONSTRUCTION EXPO KUJA NA TEKNOLOJIA MPYA.



Watanzania na Wadau mbalimbali wa Ujenzi watakiwa kujitokeza kwa wingi katika Maonesho ya Dar CONSTUCTION EXPO, ili kujifunza, nakuona  Teknolojia mpya itakayopatikana katika Sekta ya Ujenzi.


Akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi ambaye ndio Muandaaji wa Maonyesho hayo Bw. Deogratius John Kilawe amesema kuwa maonyesho hayo yanalengo la kuwakutanisha kwa pamoja wadau wa Sekta ya Ujenzi. 


Pia Mkurugenzi amefafanua kuwa maonyesho hayo yataambatana na kujadili njia mbalimbali zitakazosaidia kuinua Sekta hiyo pamoja na kukuza Mahusiano na kujipatia Wateja wa Bidhaa zao.


Pia amesema Maonesho haya   yanatarajiwa kuwa ni ya siku Tatu kuanzia  Tarehe 11- 13  Oktoba 2023  na kufanyika katika  Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dae es salaam.


Aidha Bw. Kilawe amesema kuwa, huu ni msimu wa 7 wa  Maonesho ya Dar Constructions Expo na yanajumuisha zaidi ya  Makampuni  120 kutoka nje na ndani ya Tanzania pia yanatarajiwa kuwa yenye kuleta Tija na Mapinduzi katika sekta ya ujenzi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI