Header Ads Widget

MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO KUWEKA MAWE YA MSINGI MIRADI YA AFYA NA UMEME NJOMBE

Wakuu wa Wilaya na Makatibu tawala wa Wilaya za Njombe  na Wanging'ombe

Mkuu wa mkoa wa Njombe Mhe.Antony Mtaka katikati



Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Philip Isdor Mpango anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Njombe kuanzia oktoba 24 hadi 27 mwaka huu kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ya afya, Nishati na maji.


Aidha Makamu wa Rais atashiriki zoezi la kuhitimisha maonesho ya viwanda vidogo sido yanayohusisha zaidi ya wajasiriamali 800 toka ndani na nje ya nchi.


Mbele ya vyombo vya habari Mkuu wa mkoa wa Njombe Mhe. Antony Mtaka amesema Dokta Mpango ataanza kwa kuweka jiwe la msingi katika kiwanda cha mipira ya mikono huko Idofi Makambako mkoani Njombe.


Pia Mhe.Mtaka amesema Makamu wa Rais akiwa mkoani Njombe atatembelea kiwanda cha parachichi cha Avo Afrika mjini Makambako,kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa umeme huko Makete uliopo chini ya kanisa la KKKT,Kuzungumza na wakazi wa wilaya ya Wanging'ombe huko Kipengere pamoja na kuweka jiwe la msingi katika  mradi wa maji ndani ya  halmashauri ya mji wa Njombe.


Sanjari na hayo lakini pia Dokta Mpango atatembelea kiwanda cha miwati Cha TANWATT pamoja na kuhitimisha maonesho ya viwanda vidogo SIDO hapo oktoba 27 mwaka huu.


Kutokana na ziara ya makamu wa Rais,Mtaka ametoa wito kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika mapokezi hayo.


Wakati ugeni huo wa kitaifa ukitarajia kuhitimisha maonesho ya viwanda vidogo yanayofanyika kitaifa mkoani Njombe baadhi ya wajasiriamali wanaoendelea na maonesho hayo wameiomba serikali kuwasaidia katika uongezaji thamani ya bidhaa zao pamoja na kuwawezesha kimitaji.


Kwa upande wao wakazi wa Njombe akiwemo Diwani wa kata ya Njombe mjini Alatanga Nyagawa wamesema ifike wakati sasa mazao na bidhaa wanazozalisha zipate muarobaini kwa kuzichakata hapa hapa.

Wanahabari na mkuu wa mkoa wa Njombe

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI