Header Ads Widget

MAJALIWA ATOA SABABU ZA WANANCHI WAISHIO MIPAKANI KUCHELEWA KUPA NIDA.

 


Na Mbaruku Yusuph, Matukio Daima APP Tanga. 

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa amesema muingiliano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Nchi za jirani umekuwa changamoto kubwa inayopelekea wananchi waliopo mipakani kuchelewa kupata vitambulisho vya Taifa(NIDA).


Kauli hiyo aliitoa Sep 29 alipkuwa mgeni rasmi wa kufunga mafunzo ya Askari wa uhamiaji kwenye chuo cha Uhamiaji cha Raphael Kubaga kilichopo Wilayani Mkinga ambapo Mwenyekiti wa CCM Mkoa Tanga Rajabu Abdurahman alipo omba kusaidiwa kwa wananchi wa Wilaya ya Mkinga wanaoishi mpakani na Nchi ya Kenya ambao wanakosa haki yao ya msingi ya kupatiwa vitambulisho hivyo.


Majaliwa alisema kutokana na makubaliano ya Nchi hizi ya kutoa ruhusa ya wageni kuingia Nchini na Watanzania kwenda katika Nchi hizo wapo raia toka mataifa hayo ya jumuiya ya Afrika Mashariki na nchi nyingine wanaotamani kupata vitambulisho hivyo ili wawapo Tanzania watambulike kama Watanzania. 


Alisema baadhi yao wanajua kiswahili fasaha na wanatumia mwanya huo kutafuta vitambulisho hivyo jambo ambalo ni kosa na haliwezekani kwa raia huyo wa kigeni kupatiwa kitambulisho cha Taifa hili.


"Bahati nzuri nimemaliza ziara yangu katika Mikoa ya Kagera na Kigoma ni maeneo yanayofanana na Tanga lakini moja ya malalamiko ya wananchi katika mikutano yangu ya hadhara ni swala la NIDA"Alisema Waziri Mkuu.


Waziri Mkuu alisema Serikali imejipanga vema ili kuepuka kusambaa kwa kitambulisho hicho kama kilivyosambaa kile cha mpiga kura ambapo baadhi ya raia toka Nchi za jirani walivipata kwa visingizio kuwa wao ni Watanzania. 


Alisema Serikali itaongeza timu ya uhakiki toka Jeshi la uhamiaji ili waweze kubaini kwa kila uraia aneomba kitambulisho hicho na kuongeza idadi ya watumishi toka NIDA kwenye Wilaya zote ili kukamilisha uhakiki unaofanywa ili kuwawezesha Watanzania kupata vitambulisho hivyo. 


Alisema wananchi toka katika Wilaya ya Mkinga na maeneo yote ya mipakani kwa Nchi nzima lazima watambue kitambulisho cha uraia wa Taifa kinachotolewa na NIDA ni Usalama wa Taifa na anaepaswa kupewa ni Mtanzania tu na si mtu mwengine toka Nchi jirani na ndio sababu ya Serikali kuwa makini kutokana na umuhimu wake.



"Mwenyekiti wa CCM Mkoa ulipopata nafasi ya kusalimia umelizungumzia swala la NIDA sasa nimekuongezea nondo jinsi ya kuzungumza na wananchi wako lakini hata Mbunge wa Mkinga Kitandula ambae pia ni Naibu Waziri wa Maliasili mara kadhaa amelizungumzia swala hili kule Bungeni na niwahakikishieni watanzania wote watapata vitambulisho hivyo kwani ni haki yao"Alisema Waziri Mkuu.


Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Mkoa Tanga Rajabu Abdurahman alisema kwenye ghafla hiyo ya ufungwaji wa mafunzo ya Askari hao kuwa wananchi wa Wilaya hiyo hasa wale wanaoishi karibu na mpaka wa Kenya wanakosa haki yao ya msingi ya kupata vitambulisho hivyo vya uraia wa Taifa. 


Mwenyekiti huyo alisema wakati alipofanya ziara yake Mkoa mzima wa Tanga miongoni mwa changamoto alizokutana nazo ni pamoja na wananchi wa Mkinga ambao wanaishi mpakani mwa Kenya kucheleweshewa kupatiwa vitambulisho hivyo ingawa ni kweli umakini unatakiwa wa hali ya juu ili kuepuka kutolewa kwa raia ambao si Watanzania jambo ambalo ni hatari kwa Taifa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI