Na Pamela Mollel, Arusha
Kongamano la wiki ya AZAKI kukutanisha wadau mbalimbali jijini Arusha lengo ikiwa ni kujadili, kuweka mikakati na kuboresha utendaji wa AZAKI nchi katika masuala muhimu ya Teknolojia.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, Mkurugenzi mkazi wa CBM ambaye pia ni mwenyekiti wa maandalizi ya wiki ya Azaki,Nesia Mahenge amesema kongamano hilo litasaidia kuimarisha mahusiano na ushirikiano baina ya wadau mbalimbali.
"Kupitia kongamano hili itaweza kuimarisha mahusiano na ushirikiano baina ya wadau wa maendeleo ikiwemo sekta binafsi,serikali na wananchi "alisema Mahenge.
Alisema kuwa pamoja na mambo mengine yatakayojadiliwa ni pamoja na ubunifu wa Teknolojia kwa maendeleo endelevu hali itakayosaidia kuona tumewezaje kutumia katika miradi.
"Tutaangalia mabadiliko ya kidijitali na kiteknolojia yamebadilisha mifumo yetu katika jamii kwa kiasi kikubwa na yanauwezo wakuendelea kuleta mabadiliko mengine "alisema Mahenge.
Pamoja na wageni wengine Balozi wa uswizi nchini Tanzania Didier Chassot anatarajiwa kuwa miongoni mwa washiriki wa kongamano hilo lenye kauli mbiu Teknolojia na jamii.
Mwisho
0 Comments