Tukio lisilo la kawaida, limetokea katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo mwili wa marehemu Emanuel Ngowo ulikabidhiwa kimakosa kwa ndugu wa marehemu mwingine kisha kusafirishwa.
Marehemu Ngowo ambaye mwili wake ulipaswa kusafirishwa kwenda Moshi kwa mazishi, ulisafirishwa kwenda Songea mkoani Ruvuma na kuzua taharuki kwa ndugu baada ya kubaini kuwa hakuwa ndugu yao waliyemtarajia.
Uongozi wa Hospitali ya Muhimbili, umethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuahidi kutoa ufafanuzi leo, Oktoba 20, 2023.
Wakati huohuo, familia ya Ngowo imeeleza kuwa inasubiri mwili wa ndugu yao kurudishwa kutoka Songea kwa ndege kisha waanze safari ya kuelekea Moshi.
"Ni kweli tukio limetokea hapa hospitalini kwetu, tumeliona na tumeanza kuchukua hatua kadhaa, undani wa tukio tutazungumza na wanahabari..." amesema Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma wa Hospitali ya Muhimbili, Aminiel Aligaesha.
Chanzo, GlobalTVonline
0 Comments