Header Ads Widget

DKT ANTONY KIPANGULA ACHAGULIWA KUWA ASKOFU KKKT DAYOSISI YA MUFINDI


Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo akiwa na askofu mteule wa Dayosisi ya Mufindi Dkt Antony Kipangula wakati wa harambee ya ujenzi wa kanisa la Mafinga 

WAJUMBE wa mkutano mkuu wa kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT ) Dayosisi ya Mufindi wamemchangua mchungaji Dkt Antony Kipangula kuwa askofu mteule wa Dayosisi hiyo .

Askofu  Dkt Kipangula na Msaidizi wake Askofu  Mchg Kefa Ulula wameibuka kidedea kwenye uchaguzi huo uliofanyika Leo.


Uchaguzi huo umefanyika Mufindi baada ya nafasi ya Askofu kupitishwa Kwa kupigiwa Kura NDIO NA HAPANA 

Katika uchaguzi huo kura za NDIYO zilikuwa 111 na kura za HAPANA zilikuwa 25  na hapakuwa na Kura iliyoharibika. 


Pia nafasi ya Askofu Msaidizi majina matatu yaliwekwa hadharani ambao walikuea ni Mchg Kefa Ulula, Mchg Tullo Kipingu na Mchg Zawadi Kinyamagoha. 


Katika uchaguzi huo Malibu yalikuwa Mchg Ulula alipata kura 50 ,Mchg Kipingu alipata kura 43 na Mchg Kinyamagoha alipata kura 43. 

Hata hivyo Matokeo ya upigaji wa Kura mara ya pili, na matokeo yalikuwa Mchg Ulula alipata Kura 61 Mchg Kipingu alipata Kura 35 Mchg Kinyamagoha alipata Kura 38 huku Kura Moja ikionekana kuharibika


Mara ya tatu Jina la Mchg Kipingu lilitolewa,na Mchg Kinyamagoha baada ya kujitoa na hivyo Jina la Ulula lilipigiwa Kura ya NDIYO ama HAPANA na matokeo NDIO yalikuwa ni Kura 118 na HAPANA kura 15. 


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI