Na Mbaruku Yusuph, Matukio Daima APP Kilindi
MKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba ametekeleza agizo la Rais Samia Suluhu Hassan lililomtaka atatue mgogoro wa ardhi baina ya Kijiji cha Gitu na Ngobole Wilayani Kilindi Mkoani Tanga uliodumu kwa takriban mika 17.
Hayo ameyabainisha Sept 01/2023 kwenye Mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Gitu Wilayani hapo ambapo aliwatahadharisha wananchi kuwa baada ya Mkutano huo atakaendelea kujihusisha na uchochezi wa mgogoro huo Serikali itamshughulikia kwa mujibu wa sheria.
Kindamba alisema Vitongoji vya Naroji na Komtindi kwa mujibu wa (GN) Notice ya Serikali vitaitika katika Kijiji cha Gitu pamoja na huduma zote za kijamii badala ya kuitika katika Kijiji cha Ngobole kama ilivyodaiwa hapo awali na kupelekea kuwepo kwa mgogoro baina ya Vijiji hivyo viwili.
Alisema Serikali zote mbili za Vijiji vya Ngobole na Gitu zinatakiwa ziandike Muhtasari wa maamuzi hayo ambapo Mkuu wa Wilaya hiyo atasimamia zaoezi hilo ambalo linapaswa kutekelezwa baada ya mkutano huo wa hadhara ili maamuzi hayo yawepo kimaandishi.
Mbali na hatua hiyo Mkuu huyo wa Mkoa alisema katika ardhi hiyo hekari elfu mbili zimegeiwa kwa Jeshi la wananchi JWTZ kwa ajili ya shughuli zao za Kijeshi na kufanya hivyo kutaimarisha ulinzi na usalama katika maeneo hayo.
Alisema hakuna sababu ya wananchi kugombea ardhi kwa kuwa ardhi yote imekasimishwa kwa Rais na ndio Mwenye ardhi na Mamlaka ya kuigawa kupitia GN ingawa wapo watu hawaheshimu maamuzi hayo,Serikali haitawafumbia macho kwa ukiukwaji wa taratibu zilizopo.
"Mwenyekiti wa Halmashauri na Mkurugenzi nendeni mkatengeneze vizingiti vya kutenganisha Vijiji hivyo viwili na wananchi wajue mipaka yao ili kuepusha kuzuka mgogoro mpya "Alisema Kindama.
Alisema kumekuwepo na tabia ya wananchi wa pande hizo mbili kupigana kwa kutumia silaha na kujeruhiana badala ya kuelekeza nguvu zao kuiomba Serikali kuwajemgea barabara ambayo ndio itakuwa mkombozi wa kusafirisha mazao yao na kuongezea kipato.
Katika hatua nyingine Kindamba aliwaasa Wenyeviti wa maeneo hayo waache kuuza ardhi na watambue kufanya hivyo ni kinyume na taratibu,Sheria na kanuni zilizopo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao iwapo watakaidi agizo hilo.
"Tufanyeni kazi za Nchi,viongozi wenzangu wa kuteuliwa na hata wale wa kuchaguliwa tufanyeni kazi za nchi badala ya kuwa chanzo cha migogoro"Alisema Kindamba.
0 Comments