Header Ads Widget

WAFANYABIASHARA NAZARETH WALIA NA UCHAFU

 



Na Fadhili Abdallah,Kigoma

 


WAFANYABIASHARA wa soko la Nazareth Manispaa ya Kigoma Ujiji wameeleza wanaohofia kukumbwa na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu kama ofisi ya afya ya manispaa ya Kigoma Ujiji kutoondoa uchafu unaozalishwa kwenye soko hilo kwa wakati.

 


Mwenyekiti wa soko la Nazareth , Sadoki John Akizungumza na waandishi wa habari wakati uongozi na wafanyakazi wa TPA wakifanya usafi kwenye soko hilo alisema kuwa wanawashukuru wadau hao na wadau wengine wanaojitokeza kusaidia kuweka mazingira ya soko hilo katika hali ya usafi lakini bado usafi hauna maana kama hautaweza kuondolewa na kwenda kutupwa dampo..



Mmoja wa wafanyabiashara wa soko hilo,Hussein Yassin amesema kuwa changamoto kubwa mahali kizimba cha kukusanya uchafu wote wa soko hilo kilipojengwa ambapo mvua ikinyesha uchafu wote unasombwa na maji na kuingia sokoni hivyo kuhatarisha afya za wafanyabiashara na wateja wao.




Akizungumzia changamoto hiyo Mkuu wa kitengo cha kudhibiti taka na usafi wa mazingira Manispaa ya Kigoma Ujiji,Petronila Gwakila manispaa ya Kigoma Ujiji inakabiliwa na changamoto ya kutoweza kumaliza taka zinazolishwa katika mji huo ambao taka zinazozakishwa ni tani 116 kwa siku na uwezo wa kuziondoa ni tani 74.

 


Gwakila alisema kuwa changamoto kubwa ni bajeti ndogo ya mafuta kwa ajili ya gari za kuzoa taka kupeleka kwenye dampo la Msimba nje kidogo ya mji wa Kigoma hivyo ameomba wadau ndani na nje ya nchi kuisaidia manispaa hiyo kuweza kukidhi bajeti yake kwa ajili ya usafi wa mji huo.



Akizungumza baada ya kukamilika kwa zoezi la usafi akiongoza viongozi na wafanyakazi wake Meneja wa bandari za ziwa Tanganyika wa mamlaka ya bandari TPA, Silvestre Mabula alisema kuwa zoezi hilo ni sehemu ya mchakato wa wiki ya mamlaka ya bandari kutimiza miaka 18 ambayo inahitimishwa leo.

 



Mabula alisema kuwa uongozi wa TPA na wafanyakazi wa mamlaka hiyo mkoa Kigoma wamejitolea kufanya usafi kwenye soko la Nazareth ikiwa kuunga mkono mpango wa serikali wa kutaka miji iwe safi kuwezesha shughuli mbalimbali za maendeleo na kijamii kufanyika kwenye maeneo safi na salama 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS