NA HADIJA OMARY
LINDI.......Jumla ya vijiji 16 vya halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi vinatarajiwa kuingizwa kwenye mpango wa Matumizi bora ya Aridhi
Hayo yameelezwa na Afisa Mipango Miji na Vijiji Kutoka tume ya taifa ya Mipango ya Matumizi ya ardhi Fadhili Makame Wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji Cha Chikwale halmashauri ya wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi
Mkutano huo ulilenga kutambulisha mradi wa Mpango huo wa Matumizi ya Ardhi kwenye kijiji hicho ambapo amesema kupitia mpango huo Kwa awamu ya kwanza unatarajia kuhusisha Vijiji nane.
Mpango wa Matumizi ya Ardhi katika wilaya ya Ruangwa unawezeshwa na tume ya taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa
Makame amesema vijiji hivyo ni Chiundu, Chikwale, Namkatile, Nandandala, Namkonjela, Mkaranga, Nambilanje na Nanjaru
Aidha alisema kuwa awamu ya pili vitahusika vijiji vya Namkatila , Nandandala, Namkonjela, mkaranga, Nambilanje, Nanjaru, Chiundu, Chikwale, Nangaru, Mchecha , Nandanga , Likwachu, Litama, Mibule , Chilangalile na Chikoko
0 Comments