Na Namnyaki Kivuyo - Matukio Daima App, Arusha.
Kituo cha uenezaji wa injili kwa njia mbalimbali ikiwemo Radio( Habari Maalum),mwaka 2023 imekuja kivingine katika Tamasha la kusifu na kuabudu ambapo wadau mbalimbali pamoja na wasikilizaji wamepewa fursa ya kuchagua eneo ambalo tamasha hilo litafanyika.
Tamasha hili lililobeba kauli mbiu ya “siku ya sifa 2023, jipate uweponi litafanyika Octoba 8 mkoani Arusha huku walengwa wakiwa ni watu wa Dini zote bila, rika zote, na makabila yote.
Akiongea katika kikao na waandishi wa habari leo septemba 1, meneja wa Habari maalum Lukas Kitambi alisema kuwa wataalamu wa matamasha wametoa nafasi kwa wadau wao kupendekeza eneo wanalotamani tamasha hilo lifanyike ambapo baada ya wiki moja watatangaza eneo walilochagua wadau hao.
Alisema kuwa Tamasha hilo limekuwa ni kiu ya muda mrefu na ni siku ambayo inawakumbusha kuwa Yesu kristo pekee ndiye anastahili sifa za mioyo yao hivyo siku hiyo ni kielelezo na udhihirisho wa ukuu wa Yesu.
“Niwakaribishe watu wote wa mkoa wa Arusha na mikoa ya jirani katika tamasha hili lakini pia kupendendekeza mahali litakapofanyika ikiwa ni pamoja na kuwakaribisha wadau kutoka mashirika na taasisi mbalimbali kuja kudhamini tamasha hili,” Alisema Kitambi.
Kwa upande wake Method Charles Afisa masoko wa Habari maalum media alisema kuwa awali walikuwa wakilifanya tamasha hilo kila mwaka lakini kutokana na sababu mbalimbali lilisimama kwa muda ambapo sasa limerejea na wataanzia walipoishia na kwenda mbali zaidia.
“kumekuwepo na matamsha mengi sana yaliyofanyika na kwa mfumo mmoja lakini tulikaa kimya kwa muda kidogo ili kuona ni kwanamna gani tunaweza kuja kitofauti ambapo tumegundua kuwa katika kusifu na kuabufu watu wamekuwa wakiachiliwa na matatizo mbalimbali ambayo yamekuwa yakiwakabili,” Alisema.
“Siri ipo kwenye kusifu na kuabudu na kwa kulifahamu hilo tukutane October 8 kwasababu kupitia njia hiyo Mungu anatekeleza mahitaji yetu wakati tumejiachia kwake,” Alieleza.
Naye mratibu wa Tamasha hilo Goodluck John alieleza kuwa maandalizi ni makubwa na watahakikisha wanakuja na kitu kizuri kwani wamegundua ni kitu gani watu wanahitaji lakini pia katika tamasha hilo litakuwa na t shirt maalumu ambazo kila atayehitaji anaweza kuwasiliana na kituo hicho.
0 Comments