.
NA NAMNYAKI KIVUYO ,ARUSHA.
Wakala wa usalama na Afya mahala pa kazi(OSHA) imewakutanisha mkoani Arusha wabunge wa kamati ya kudumu ya bunge ya bajeti katika mafunzo maalum ya usalama na Afya mahala pa kazi.
Akifungua Mafunzo hayo leo Septemba 10 Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu Prof Joyce Ndalichako alisema kuwa ili kuendelea kulinda afya na usalama wa wafanyakazi, wana wajibu mkubwa wa kushirikiana na kuimarisha mifumo ya usimamizi wa afya na usalama kwani wao ndio nguvu kazi inayotegemewa kwa maendeleo ya nchi.
Prof Ndalichako alisema kuwa masuala ya afya na usalama ni masuala mtambuka na yanagusa sekta zote za uchumi hivyo wautambue kuwa ulimwengu wa kazi unakabiliwa na vihatarishi vingi vitokanavyo na ukuaji wa uchumi,mabadiko ya teknolojia na ushindani wa kibiasharaambapo yote hayo yanahitaji mbinu mpya au mbadala wa kuweza kubaini na kuthibiti athari ya vihatarishi hivyo.
Alifafanua kuwa katika kulinda nguvu kazi ya taifa pamoja na uwekezaji uliopo nchini, OSHA ina jukumu la kukagua maeneo ya kazi na kufanya uchunguzi wa afya za wafanyakazi ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya namna ya kukabiliana na kuthibiti ya viatarishi hivyo.
Alieleza kuwa serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji na waajiri ili waweze kuleta ajira na kuchangia kukuza pato la taifa ambapo hivi karibuni serikali kupitia OSHA imeondoa tozo 13 ili kupunguza kero ikiwa na nyingine nyingi kupunguza gharama mojawapo ikiwa ni kupunguza tozo ya umeme katika vituo vya mafuta vijijini kutoka 650000 hadi kufikia 150000.
“Tozo hizi zilizofutwa na kupunguzwa na OSHA zimeweza kuleta unafuu kwa wafanyabiashara na wawekezaji nchini kwa kuwapunguzia ghara za uendeshaji kwa kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 35 endapo zingeendelea kutozwa,” Alieleza.
kwa upande wake katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu kazi,vijana, ajira na wenye ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja alisema kwa takwimu za shirika la afya duniani inaonyesha kuwa kwa mwaka takribani watu 2,300,000 wanakufa kutokana na ajali mahala pa kazi ambapo kwa hapa nchini kwa kipindi chamwaka mmoja Julai,2020/2021 ajali zilizoripotiwa zilikuwa 1889 kati ya hizo vifo vilikuwa 7500.
“Kutokana na ajali hizi mahala pa kazi gharama za fidia zimeongezeka kutoka bilioni 13.19 kwa kipindi kilichoishia June 2021 hadi kufikia bilioni 17.93 kwa kipindi kilichoishia Juni 2023, hivyo kuna haja ya kuhakikisha gharama hizi na madhila vinapungua kwa kila muajiri kusimika mifumo ya Afya na usalama mahala pa kazi,” Alisema.
Naye mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya bajeti Daniel Sillo(MB) alisema kuwa wanashukuru kwa mafunzo hayo ambayo yatawawesha kupata uelewa zaidi na kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa suala hilo kwani wanapokuwa na jamii au wafanyakazi wenye afya tija inaongezeka.
Mtendaji mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda alisema kuwa viatarishi ni vingi sehemu za kazi ambapo mafunzo hayo yatawaoshe moja kwa moja viatarishi hivyo ikiwa ni pamoja na mifumo ya kuthibiti viatarishi hivyo.
0 Comments