Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma
WAZIRI wa Habari , Mawasiliano naTeknolojia ya Habari Nape Nnauye ameombwa kuingilia Kati Suala zima la utapeli kwa njia ya mitandao ya kijamii ambalo limeonekana kuwaumiza wananchi wa hali ya chini kutokana na kukopa Fedha kwenye akaunti feki.
Hayo yameelezwa Jijini Dodoma na baadhi ya Wananchi walipokuwa wakiongea na Matukio Daima Blog baada ya kuja na kueleza Maombi yao kwa Waziri mwenye dhamana kuwasaidia Watanzania ambao bado hawajakumbwa na utapeli huo kwa njia yatandao.
Eliwaza Kusulya ni mkazi wa MTUMBA jijini Dodoma hapa anaeleza machungu yake baada ya kutapeliwa Fedha na matapeli hao TALA TANZANIA.
"Nilikuwa ninauhitaji wa Shilingi 200,000
Lakini nilipokuwa nachati Katika mtandao mmoja wa kijamii wa Facebook ndipo nilupoona mkopo wa kampuni ya TALA TANZANIA na nuliposoma masharti yake nikavutiwa na nikaanza kuwasiliana nao Ni kweli walinipa fomu nikajaza na kutuma akiba zangu kiasi Cha Shilingi 20000," Amesema
Na kuongeza" kwenye fomu yao ya Maombi walisema ukituma akiba unapata Fedha ya mkopo ndani ya dakika 30 lakini baada ya kutuma nikaona masaa yanakatima na nilivyojaribu kupiga namba iliyonipigia na kujitambulisha Kama meneja ilikuwa haipatikani nasikitika Sana ilikuwa ni hela ya biashara lengo la mkopo ilikuwa Ni kuongeza mtaji kumbe ni matapeli TALA TANZANIA sio wakopeshaji ni matapeli," Amesema Eliwaza huku akilia kilio Cha kwikwi..
Naye Tatu Salumu Mkazi wa Mailimbili kwa mudi amesema TALA TANZANIA walifanya niambulie makofi kwa mume wangu baada ya kutuma Fedha nilioachiwa ya Chakula .
" Nilivyoona akiba Shilingi 19500 unapokea Shilingi 100,000 ndani ya dakika 30 nikahamasika na kutuma Fedha hiyo kumbe nimewapatia ulaji matapeli iliniuma Sana nawapigia simu hawapatikani mume anarudi Sina hela Hakuna Chakula ndani siku hiyo mume wangu alinipiga Sana baada ya kukuta Hakuna Chakula na hela aliniachia asubuhi "Amesema
Na kuongeza" kunahaja Sasa ya makampuni ya simu kuweka utaratibu mzuri wa mtu kusajili laini zaidi ya mbili kwani hao Matapeli TALA TANZANIA wanatumia namba za simu tofauti tofauti na baada ya kumtapeli mtu wanamblok na ukipiga simu yao haipatikana na ikipatikana hawapokei tunaomba serikali iingilie Kati Suala hili Watu wanalizwa na mikopo holela mitandaoni," amesema Tatu.
0 Comments