Na Simon Joshua - MAtukio Daima App, Johannesburg.
Raia wa Tanzania Mussi Hamisi aliamshwa na sauti ya kishindo kikubwa. Kitanda chake kilikuwa kinatikisika na alisikia watu wakipiga kelele: "Moto! Moto! Moto!"
Kwa mshtuko, alipofungua macho aliona mwanga wa rangi ya chungwa wa miali ya moto ukiingia kwenye nyumba yake ya muda kwenye ghorofa ya tatu ya jengo hilo, lililokuwa likimilikiwa na jiji la Johannesburg, ambalo lilikuwa makazi yasiyo rasmi ya wahamiaji.
Bwana Hamisi alimtoa mke wake na mtoto wao wa mwaka mmoja kitandani. Aligundua kuwa nafasi yao pekee ya kuishi ilikuwa kuruka nje ya dirisha.
Ilikuwa ni kutua juu ya saruji iliokauka , alipata majeraha .Lakini yuko hai.
Mke wa Mr Hamissa alimshusha mtoto wao dirishani na Hamisa akampokea salama.
Mkewe kisha akafunga shuka kwenye sahani ya satelaiti na akajishusha chini.
"Watu walianza kutuiga. Waliruka, lakini hawakufanikiwa," alisema, macho yakiwa yamemtoka.
"Kulikuwa na maiti nyingi... Miili mingi sana. Na sikuweza kuwasaidia."
Bwana Hamisi, kutoka Tanzania, alikuwa ameishi katika jengo hilo kwa miaka mitatu. Alijua Watanzania wengine wote katika jengo la ghorofa na alisema wengi wao hawakufanikiwa.
"Nilipoteza kaka na dada wengi. Familia yangu. Wote walikuwepo, lakini ningeweza tu kuokoa mke wangu na mtoto."
Hatia itasalia naye milele, alisema.
Familia hiyo pia ilipoteza pesa zao, pasipoti na mali zao zote.
Akiwa anaishi katika jengo hili kama skwota, Bw Hamisi hakulazimika kulipa kodi. Na sasa kwa kuwa hati zake muhimu zimepotea na kazi yake ni ya malipo ya chini, hajui cha kufanya na wapi pa kwenda .
Kwa hivyo ameketi katika barabara iliopo katika jengo alilokuwa akishi , moshi ungali unafuka kutoka kwa mabaki yake , akitumaini tu kwamba atapata eneo la kulala kwa ajili ya mwanawe usiku wa leo.
"Sijui watatufanya nini, serikali inapaswa kutusaidia kwa sababu tulipoteza vitu vyetu vyote," alisema.
Wengi hawakubahatika kuliko bwana Hamisi.
Sphiwe Ngcobo alikuwa nje ya jengo kwenye kibanda chake cha biashara wakati moto ulipozuka. Ni tukio lililofanyika kwa haraka sana, anasema, kwamba wakati alipovuka barabara hadi kwenye jengo hilo, miali ya moto ilikuwa tayari imeziba njia.
Alikuwa na watoto wawili ndani - wote kwenye ghorofa ya pili, wote hawakuweza kufikiwa.
Bi Ngcobo alisubiri kwa saa nyingi watu walipoanza kuokolewa kutoka kwa jengo lililokuwa likiungua.
Hatimaye mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka mitano aliokolewa na jirani .
Alikuwa akitokwa na povu mdomoni. Alikuwa amevuta moshi mwingi na alikuwa katika hali ya mshtuko kiasi kwamba alishindwa kusimama bila msaada.
Wahudumu wa afya walimpeleka hospitalini na hajasikia kuhusu hali yake tangu wakati huo.
Bi Ngcobo alibaki nyuma, akisubiri katika eneo la moto kwa taarifa zaidi kuhusu mahali ambapo mwili wa mtoto wake wa miaka miwili umepelekwa.
Anataka kuuaga mwili wake.
"Sijui la kufanya, sijui niende wapi," alisema. "Sijui mtoto wangu yuko hospitali gani, na sijui mtoto wangu mwingine yuko katika chumba gani cha kuhifadhia maiti. Kwa hiyo nitasubiri habari hapa."
Bwana Hamisi na Bi Ngcobo walikuwa wamekaa kwenye kundi la watu takriban 50, wote wakijaribu kupata usingizi huku wakisubiri viongozi wawaeleze kitakachotokea.
Kulikuwa na uvundo hewani wa moshi wa zamani na chakula kilichoisha muda wake. Njia ya lami ilikuwa imejaa takataka na vitu tofauti tofauti .
Kwa sasa, hapo ndipo watakaa.
0 Comments