MMOJA kati ya Mashahidi wa mwisho wa mauaji ya Rapa Tupac Shakur yaliyotokea mwaka 1996 aliye hai kwa sasa amekamatwa katika eneo la Las Vegas, nchini Marekani katika tukio ambalo lilikuwa likisubiriwa kwa muda mrefu zaidi ikiwa ni moja ya kesi ambayo imewakatisha tamaa Wachunguzi na kuvutia umma tangu Msanii huyo wa Hip-hop auawe baada ya kutoka kwenye mechi ya boxing miaka 27 iliyopita.
Duane "Keffe D" Davis amekamatwa mapema hii leo kwa tuhuma za mauaji na atasomea mashtaka, hii ni kwa mujibu wa Maafisa wawili wanaojua moja kwa moja taarifa za kukamatwa kwa Mshukiwa huyo ila Maafisa hao waliomba kutotajwa majina yao.
Miezi miwili iliyopita Mahakama iliorodhesha hati iliyoruhusu upekuzi wa nyumbani kwa Mke wake Davis huku Mamlaka ikidhamiria kutafuta ushahidi wa mauaji ya Tupac Shakur na kulingana na ripoti ya Polisi walikusanya computer kadhaa, simu za mkononi na cd kadhaa, risasi kadhaa za caliber 40, jarida la ‘vibe’ likiwa na picha mbili za Tupac na nakala ya kumbukumbu ya Davis.
Katika nakala yake, Davis alisema alikuwa amekaa kwenye kiti cha mbele katika gari aina ya Cadillac nyeupe iliyokuwa na muuaji wa Tupac kisha akachukua bunduki iliyotumika katika mauaji hayo na kuirusha kuelekeza kwenye kiti cha nyuma, ambapo amesema ndipo risasi zilipofyatuliwa, Tupac alikuwa kwenye gari aina ya BMW na alishambuliwa na risasi kadhaa ikapelekea kifo chake akiwa na miaka 25.
Wakati huo Shakur alikuwa kwenye mzozano na Mpinzania wake kwenye game ya rap Notorious BIG ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi mwezi Machi 1997.
0 Comments