Kumekuwepo na mijadala mbali mbali kwenye vyombo vya habari vya mtandaoni hususani makundi ya WhatSApp juu ya taarifa za kukamatwa kwa muingereza huyu mwenye asili ya Tanzania mzaliwa wa mkoa wa Iringa .
Kutokana na Sintofahamu hiyo timu ya matukio Daima media imelazimika kufunga safari kutoka mkoani Iringa Zaidi ya kilomita 500 hadi jijini Dar es Salaam ofisi za Uhamiaji Taifa ili kupata ukweli wa sakata hili.
Kamishna wa Paspoti na Uraia Gerald Kihinga ni Kamishna wa Paspoti na Uraia anakutana na timu ya waandishi wa habari kwa niaba ya kamishna mkuu wa Uhamiaji Taifa Anna Makakala ambae kwa wakati huo alikuwa nje ya jiji la Dar es Salaam kwa majukumu ya kikazi .
Kihinga alisema Mlowe ambae anafahamika kama Namlowe ni kweli anashikiliwa uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere kwa kutaka kuingia nchini bila kibali cha waziri wa mambo ya ndani ya nchi.
“Namlowe alipoteza sifa ya kuwa Mtanzania baada ya kwenda nchini Uingereza na kupata paspoti ya nchi hiyo yenye namba GBR- 562745957 inayokwisha muda wake Oktoba 10, 2029” alisema
Kamishna Kihinga alisema Mlowe amekuwa na tuhuma nyingi za kiuhamiaji pamoja na makosa mbalimbali ya kijinai kama vile kughushi nyaraka za serikali na kuwatukana viongozi wa serikali kwenye mitandao ya kijamii na kujishughurisha na siasa wakati yeye si raia wa Tanzania.
Anaendelea kusema kuwa mwaka 2018 Mlowe alifikishwa Mahakamani kwa kosa la kumiliki paspoti mbili, kughushi nyaraka, kujihusisha na siasa na kwamba alikiri makossa kwenye kesi namba 306 ya mwaka 2018 katika Mahakama ya Kisutu na alihukumiwa kifungo au faini ya shilingi 630,000.
“Mlowe alilipa faini hiyo hivyo kwa kuwa yeye ni raia wa nje alikiri makossa Makahamani tukamuondosha nchini kwa sababu anatuvurugi amani ya nchi yetu kwa hiyo alirudi kwao Uingereza,
Sasa tukashangaa tarehe 30 Agosti 2023 kupitia shirika la ndege la Ujerumani (KLM) namba KLM 569kupitia uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere alirejea nchini. Hivyo tumemuamuru arudi nchini kwao hatutaki vurugu katika nchi yetu”. Alisema Kamishna Kihinga.
Kamishna Kihinga alisema mtu akishakuwa na makosa ya jinai uwezi kumruhusu kuingia nchini bali nchi ndiyo yenye mamlaka ya kumruhusu aingie au asiingie hata hivyo amepewa taratibu kama anataka kuingia ni lazima aombe kibari kwa Waziri wa Mambo ya Ndani lakini siyo yeye kufanya fujo ya kulazimisha aingie sharia hairuhusu.
“Kwa sasa yupo uwanja wa ndenge amezuiliwa kuingia nchini lakini kunakitu alighushi katika mifumo yetu tuliweza kumzuia alichokifanya alikwenda kubadilisha sehemu ya kuzaliwa alisema kazaliwa Burundi na siyo Tanzania kwa hiyo baada ya kubaini yote haya hatuwezi kumruhusu kuingia huyo ni mharifu wa Kimataifa”. Alisema Kamishna Kihinga.
Akizungumzia suala la kwamba Mlowe ni moja kati ya watalii walioitikia wito kupitia jitihada za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuzunguka kutangaza utalii kupitia filamu ya Royal Tour ,Kamishna Kihinga alisema huyo siyo mtalii kwani mtalii aghushi nyaraka huyo ni mharifu wa makossa ya jinai hatakiwi nchini.
Hata hivyo alivyoulizwa kuhusu Uhamiaji kutumika vibaya kwa kutumiwa kuingiza masuala ya idara hiyo na masuala binafsi ya ugomvi wa kifamilia kati yake na mzazi mwenzake ofisa huyo alisema si kweli Uhamiaji inafanya kazi yake kwa mujibu wa sharia na si vinginevyo.
Kukamatwa kwa Michael Mlowe kumekuwepo na mijadara mbalimbali katika mitandao ya kijamii wakimshutumu Kamishna Mkuu wa Uhamiaji nchini Anna Makakala kutumika kumkandamiza Mlowe kupitia ofisi ya uhamiaji, katika moja ya kauli yake Michaele Mlowe kwenye mitandao ya kijamii alinukuliwa akisema hana ugomvi na mzazi mwenzake wala ofisi ya uhamiaji anaheshimu taifa lake Tanzania na wala hana ugomvi na idara ya usalama wa Taifa.
“Mimi sina ugomvi na mzazi mwenzangu, ofisi ya Uhamiaji wala Idara ya Usalama wa Taifa naiheshimu nchi yangu Tanzania”. Alisema Mlowe.
Jitiahda za kumtafuta waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mhandisi Hamad Masauni bado zinafanyika ili kujua hatima ya Namlowe kutembelea nchi ya Tanzania endelea kufuatilia undani wa sakata hili.
PAKUA APP YA MATUKIO DAIMA AMA TEMBELEA CHANEL YA MATUKIO DAIMA TV KUONA VIDEO NZIMA
0 Comments