Header Ads Widget

BABA WA MWIMBAJI ALIYEIMBA MNATUONA NYANI TU AFUNGWA JELA ,KWA KOSA HILI..

Na Matukio Daima Media, Mbeya 

MCHUNGAJI Mbarikiwa Mwakipesile (39)Baba wa mwimbaji wa nyimbo za injili Sifa  Bujune aliyeimba wimbo  wa "Mnatuona Nyani Tu "amehukumiwa  kifungo cha miaka mitatu jela na Mahakama  ya Hakimu Mkazi Mbeya kwa kosa la kukutwa akiendesha kikosi kazi cha Injili bila usajili.


Hukumu hiyo imetolewa leo na  Hakimu Mkazi Mku Mkuu Paul Ntumo ambapo amesema  Jamhuri ilikuwa ikimshtaki Mchungaji Mbarikiwa kwa kuendesha jumuia ya Kikosi kazi cha injili bila usajili .


Hakimu Ntumo amesema maelezo  hayakubishaniwa na uoande wa utetezi ambao ulidai unaendelea na taratibu za usajili huku wakiendelea kukutana kwa ajili ya huduma ya maombi.


Hata hivyo kwenye utetezi wake Mch. Mwakipesile aliiomba Mahakama Serikali kumuongezea muda kwani anaendelea kushughulikia taratibu za usajili wa Kikosi kazi cha Injili ambao wamekuwa wakikutana kama jumuia kwa ajili ya maombi pekee ushahidi ambao pia ulitolewa na mashahidi wake hasa waumini wa jumuiya ya Kikosi kazi cha Injili


Aidha Hakimu  Ntumo ameeleza kuwa upande wa Mashtaka umethibitisha bila kuacha shaka mshtakiwa huyo kwamba alikuwa akiendesha shughuli za jumuiya ya kidini bila kuisajili ushahidi ambao ulielezwa na mashahidi mbalimbali wa Jamhuri kwa nyakati tofauti wakati wa kusikilizwa kwa shauri hilo..


Hata hivyo Mawakili Elisia Paul na Dominic Mushi ndio walikuwa waendesha mashtaka wa Serikali ambapo wakili Mushi ameiomba mahakama kutoa adhabu kama sheria inavyoelekeza ili iwe fundisho kwa mshtakiwa na watu wengine kwenye jamii kwa kukiuka sheria makusudi wakati akijua kuendesha huduma bila usajili .


Amesema kuwa ni kinyume cha sheria na Mchungaji Mbarikiwa alikuwa akiwakilishwa na wakili Boniface Mwabukusi ambaye hata hivyo hakuwepo Mahakamani kwenye usomwaji shauri hilo.


Hata hivyo imeelezwa kuwa mchungaji huyo baada ya kutiwa hatiani  aliiomba Mahakama kumpunguzia adhabu kwani ni mkosaji wa mara ya kwanza na alikuwa akiendelea na taratibu za usajili wa huduma ya kikosi kazi kuwa kanisa kamili na ni mtumishi anayetegemewa .


Aidha baada ya kuridhika na ushahidi wa Jamhuri na utetezi pia maombolezo ya Mtumishi huyo, Hakimu Paul Ntumo amemhukumu Mchungaji Mbarikiwa Dickson Mwakipesile (39) mkazi wa Isyesye jijini Mbeya kwenda kutumikia kifungo cha miaka mitatu  jela na siku 14 jela na kuweka wazi haki ya kukata Rufaa kwa upande usioridhika na hukumu hiyo.

Kosa alilokuwa akituhumiwa Mchungaji huyo na sasa limeelezwa kuthibitishwa ni kinyume na kifungu namba 25 (1) cha sheria ya usajili wa Taasisi za kijamii sura namba 337 kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2019.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI