Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP DODOMA
KUTOKANA na kuwepo kwa wimbi la utoroshaji wa Madini nje ya nchi Waziri wa Madini,Anthony Mavunde amesema hataangalia sura ya mtu Wala cheo na badala yake kwa yeyote atakayebainika sheria itafuata mkondo wake.
Mavunde ameyaeleza hayo Leo Septemba 11,2023 Jijini Dodoma wakati wa kikao Cha pamoja kati ya Wachinbaji wadogo chini ya MwamVuli wa FEMATA.
Amebainisha kuwa ili kuhakikisha Nchi inanufaika na rasilimali za Madini Nchini hatakuwa na huruma kwa mtu yeyote atakayebainika anatorosha Madini nje ya Nchi hatasita kumchukulua hatua za Kisheria.
"Najua Kuna utorosha mkubwa sana wa Madini lakini Kuna kazi kubwa inayofanyika ya kuzuia Vitendo hivyo ili nchii iweze kunufaika na Madini kutokana na Dhamana niliyopewq lazima nisimamie Sheria,"Amesema
Aidha ameeleza kuhusu suala la Mikakati ambayo ataitekeleza ambayo ni Ajenda ya 2030 Madini ni maisha a utajiri ambapo ataijengea uwezo Taasisi ya jiolojiana utafiti wa Madini nchini GST kwani huo ndio Moyo wa Madini kuhakikisha inafanya utafiti wa Madini ili kutoa taarifa sahihi za kijilojia na kuweza kufikia malengo yao.
Ili kufanya utafiti huo ,mwelekeo wake chini ya maelekezo ya Rais anataka kufanya survey katika maeneo yote ili kupata taarifa za jiolojia maeneo yote yenye miamba na uwepo wa Madini na kutimiza azma ya Serikali katika ukuaji wa Sekta hiyo.
Pamoja na hayo amesema atahakikisha Wachinbaji wadogo wa Madini wanakopesheka ili kuweza kunufaika na kazi zao.
Katika hatua nyingine Mavunde amesema kuwa kutokana na kazi kubwa inayofanyika na GST wataijenga Maabara ya kisasa ili kuweza kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
Naye Rais wa Shirikisho la Wachimbaji wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA)John Bina ameeleza changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo suala la Kodi kubwa ya tozo na kushuka kwa bei ya Tanzanite.
"Mheshiniwa Waziri tunaomba kupitia wewe Serikali itusaidie kutatua changamoto hizi za tozo pamoja na gharama kubwa ya umeme pia tujengewe Hospitali pale Merelani kutona na uwepo wa vumbi,"amesisitiza.
0 Comments