Header Ads Widget

MAKAMU WA RAIS AHUTUBIA BARAZA KUU LA 78 LA UMOJA WA MATAIFA


Matukio Daima App, Marekani.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip   Mpango  amesema  kwa   sasa   dunia   inashuhudia   kufifia   kwa mshikamano thabiti wa kihistoria, udugu na kujitolea, kutoingiliana, usawa baina ya mataifa na kunufaishana uliowekwa na  waanzilishi wa Umoja wa Mataifa.


Makamu wa Rais amesema hayo wakati akihutubia Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaofanyika Makao Makuu ya Umoja   wa   Mataifa   Jijini   New   York   nchini   Marekani.   Amesema   ili kurejesha imani na mshikamano baina ya mataifa ni vema mataifa yaliyoendelea   kuhakikisha   yanatimiza   ahadi   zake   na   sauti   za mataifa yanayoendelea zinasikilizwa. 


Amesema kumekuwepo na kutoaminiana baina ya mataifa na hivyo kupelekea   mmomonyoko   wa   utawala   wa   sheria,   mataifa   kuunda miunganiko tofauti na ile ya asili pamoja na kurejea kwa maamuzi ya   upande   mmoja.   Ameongeza   kwamba   kwa   sasa   kumekuwa   na maswali zaidi juu ya ufanisi wa Mfumo wa Umoja wa Mataifa pamoja na Taasisi za Fedha za kimataifa zikihitajika kufanyiwa maboresho ya haraka.

Makamu   wa   Rais   amesema   Umoja   wa   Mataifa   unapaswa kuwakemea   kwa   uwazi   wale   wote   wanaoshiriki   katika   kuchochea migogoro barani Afrika kwa lengo la kuuza silaha au kupata utajiri wa rasilimali zilizopo. Ameongeza kwamba dunia inahitaji kuwekeza zaidi katika mazungumzo na diplomasia katika kutatua migogoro ya kivita   ili   kuifanya   kuwa   sehemu   salama   kwa   vizazi   vya   sasa   na vijavyo. 


Halikadhalika   Makamu   wa   Rais   amesema   Tanzania   itaendelea kuchangia katika juhudi za kuleta na kudumisha amani barani Afrika na   kwingineko   duniani   na   kutoa   wito   kwa   jumuiya   ya   kimataifa kuongeza   uungaji   mkono   katika   mipango   ya   kikanda   ya   kuleta amani   katika   maeneo   yenye   vita   barani   Afrika.   Amesema   hadi kufikia   mwezi   machi   2023   Tanzania   imekua   ndio   mchangiaji mkubwa wa 12 kati ya nchi 125 katika shughuli za Umoja wa Mataifa za kulinda amani. 


Makamu wa Rais amesema utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu   umekuwa   wa   kukatisha   tamaa   hasa   kutokana   na kutotekelezwa kwa ahadi za kifedha na teknolojia kutoka kwa nchi zilizoendelea   duniani na upungufu wa fedha katika nchi nyingi za Afrika.

Amesema Tanzania imedhamiria  kutekeleza  kikamilifu malengo ya maendeleo enedelevu   kama inavyotarajiwa ambapo   Julai mwaka huu   iliwasilisha   Ripoti   ya   pili   ya   Hiari   ya   Taifa   (VNR)   ambayo inaonyesha   kwa   ujumla   kumekuwa   na   mafanikio   makubwa   kwa lengo   namba       2–7   kwa   ongezeko   la   uwiano   wa   kutosha   wa chakula, upatikanaji wa dawa muhimu, kupungua vifo vya chini ya miaka   5,hatua   muhimu   katika   kuhamasisha   usawa   wa   kijinsia, uboreshaji wa upatikanaji wa maji mijini na vijijini pamoja na utoaji wa huduma ya nishati ya umeme. Ameongeza kwamba pamoja na kuwepo   kwa   utendaji   wa   wastani   katika   lengo   namba   1,8   na   10, Tanzania   imedhamiria   kuchukua   hatua   kuboresha   zaidi   juhudi   za mapato   ya   ndani   huku   ikitumia   mfumo   wa   ushirikiano   baina   ya serikali   na   sekta   binafsi   pamoja   na   kuweka   kipaumbele   kwenye uwekezaji katika sekta za huduma za jamii, kilimo na biashara ya kilimo, uongezaji thamani na miundombinu, pamoja na kuinua ujuzi wa vijana.


Kuhusu mazingira, Makamu wa Rais amesema Tanzania inasisitiza wito   wake   wa   kuchukua   hatua   za   haraka   na   za   pamoja   za kupunguza   uzalishaji   wa   gesijoto   pamoja   na   kuimarisha   hatua   za kukabiliana   na   hali   hiyo.   Amesema   ni   lazima   kuweka   mazingira wezeshi na kuwezesha uwekezaji unaohitajika ili kutumia rasilimali kwa ajili ya kuongeza utekelezaji wa ahadi zinazohusu mabadiliko ya tabianchi   na   uondoaji   wa   kaboni   katika   uchumi   wa   dunia.   Aidha amesema   Tanzania   inasisitiza   wito   wake   wa   mabadiliko   ya   haki katika kukia nishati sa kwa nchi za Afrika.


Makamu wa Rais amesema Tanzania imeendelea kuwa imara katika kupinga dhuluma popote inapotendeka na kwa yeyote yule. Ametoa wito wa kuondolewa kwa vikwazo vya kiuchumi visivyo vya haki kwa mataifa kwani vimekua vikidhoosha uhuru na ustawi kwa wote.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS