Header Ads Widget

KUMEKUCHA MASHINDANO YA RIADHA TAIFA 2023

 



NA TULLO CHAMBO, RT

JOTO la mashindano ya Riadha ya Taifa 2023 yanayotarajiwa kurindima mkoani Morogoro kuanzia Septemba 29-30, limezidi kupanda baada ya kutolewa kwa orodha ya mikoa na idadi ya washiriki 'kota'.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Wakili msomi Jackson Ndaweka, mikoa 31 ya Tanzania Bara na Zanzibar inatarajiwa kushiriki.

Wakili Ndaweka, alisema mashindano hayo ni muhimu kwa mustakabali wa mchezo wa Riadha, hasa ukizingatia mwakani kutakuwa na matukio mengi makubwa kimataifa.

Katika orodha hiyo iliyotolewa, mikoa ya Kusini Unguja, Arusha, Kilimanjaro na Dar es Salaam inaongoza kwa kupewa nafasi za wachezaji 15 na viongozi wawili kila mmoja.

Mikoa inayofuatia ni Singida, Tanga na Tabora yenye wachezaji 10 kila mmoja na viongozi wawili.

Mkoa unaofuatia ni Kaskazini Unguja wachezaji saba, Mjini Magharibi sita huku Kaskazini Pemba na Kusini Pemba zikiwa na wachezaji watano kila mmoja na kiongozi mmoja.

Mikoa mingine yote iliyosalia imepewa nafasi ya wachezaji wawili na kiongozi mmoja kila mmoja, isipokuwa mwenyeji Morogoro ambaye yuko huru kwa idadi ya washiriki.

Awali, RT iliitaka mikoa kuendesha mashindano ya majaribio na kutuma matokeo kwenye shirikisho, kwani ndio itakuwa moja ya kigezo cha ugawaji kota.

Mashindano hayo yanakuja ikiwa ni kiu ya muda mrefu ya mikoa, hivyo yanatarajiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI