Header Ads Widget

CCM YAIBUKA KIDEDEA UCHAGUZI MDOGO WA MARUDIO KATA ZA MARANGU KITOWO NA OLD MOSHI MAGHARIBI.



NA WILLIUM PAUL, KILIMANJARO.

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka mshindi katika uchaguzi mdogo wa marudio ya Udiwani katika kata za Old Moshi magharibi wilayani Moshi na Marangu kitowo wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro.


Uchaguzi huo uliofanyika jana ambapo katika kata ya Old Moshi magharibi kulikuwa na wagombea wa vyama saba ambao ni Peter Massawe (CCM) aliyepata kura 3538.


Wagombea wengi na idadi ya kura walizopata ni Florence Saria (SAU) kura 38, Stephen Machange (NCCR Mageuzi) kura 81, Edward Mosha (ADC) kura 23, Luckresia Mkenda (ADA-TADEA) kura 11, Elisaria Macha (DP) kura 13, na Samweli Owenya (NRA) kura 14.


Katika kata ya Marangu kitowo wilayani Rombo kulikuwa na wagombea watano ambapo mgombea wa Chama cha Mapinduzi Simon Massawe aliibuka mshindi kwa kupata kura 1659.


Wagombea wengi kata kata hiyo ni Dionis Shirima (SAU) alipata kura 101, August Baimu (ADA -TADEA) kura 12, Nestory Kimario (DP) kura 15, na Clemence Kimario (TLP) kura 6.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI