ASKOFU wa kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Ruaha Joseph Mgomi amewataka waumini wa Kanisa hilo kujiepusha na imani zenye mmomonyoko wa maadili .
Akizungumza Leo wakati wa Ibada ya uzinduzi wa Kongamano la kitaifa la utume na uinjilisti Anglikana Tanzania linalofanyika ukumbi wa chuo kikuu cha Mkwawa Iringa ,Askofu huyo alisema sifa Kubwa ya mtumishi wa Mungu ni uaminifu.
Alisema wapo baadhi ya Watu ambao wanajivisha vyeo vya kila aina Ili kuwavuta waumini kwa maslahi yao jambo ambalo SI Sawa.
Kuwa suala la mmomonyoko wa maadili kwa jamii limeendelea kuchochewa na imani potofu na Sasa wapo ambao wanahamasisha Ndoa za jinsia Moja na Mambo mengine yasio faa kwenye jamii .
Hivyo alisema ni wajibu wa wainjilisti na watumishi wa kweli wa kanisa kupinga mafundisho yote yasiyo faa.
0 Comments