Header Ads Widget

CCM NJOMBE YAAGIZA SERIKALI KUKOMESHA MATUKIO YA UJAMBAZI NA MAUAJI

 


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE 


Kufuatia kukithiri kwa matukio ya Wizi, Ujambazi na mauaji yanayowalenga wafanyabiashara hususani wanaojihusisha na biashara ya fedha, Mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama  kutekeleza majukumu yao ipasavyo  ili kudhibiti vitendo hivyo kabla havijatokea na kuathiri wananchi kama ilivyotokea siku chache zilizopita.


Mtaka ametoa agizo hilo kufuatia ushauri wa CCM katika kikao cha halmashauri kuu ya CCM Mkoa wa Njombe cha kujadili mwenendo wa mkoa kwasasa na kisha kutoka na maadhimio ya kwenda kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi ambapo amesema kwakuwa yeye ndiyo mwenyekiti wa ulinzi na usalama mkoa hivyo hatavumilia kundi la majambazi kuteka watu ,Kupora na kufanya mauaji hivyo kila mtu atekeleze majukumu yao ili kuweka usalama wa watu jambo linalotiliwa mkazo na mwenyekiti wa CCM mkoa ambaye ni mbunge wa jimbo la Makambako Mhe.Deo Sanga.



Kwa kuwa moja ya maazimio katika kikao hicho ni kutatua kero za wananchi ,wabunge wa mkoa wa Njombe nao akiwemo Deo Mwanyika ,Joseph Kamonga na Edwin Swalle wameweka bayana changamoto kubwa zinazopigiwa kelele na wananchi katika majimbo yao ambazo ni maji,Umeme,barabara pamoja ukosefu wa mafuta ambapo wanasema wamejipanga kwenda kuzitatua. 


Wakati wabunge wakiweka bayana nini cha kufanya ili kupata ufumbuzi wa kero za wananchi ,Mkuu wa mkoa Pia anazitaka taasisi za serikali na viongozi mbalimbali wa serikali kutumia vyombo vya habari kueleza kinachofanywa na serikali badala ya kusubiri wakati wa uchaguzi.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS