Header Ads Widget

ZFF IMEKANUSHA TAARIFA ILIYOTOLEWA NA NEW GENERATION

 


NA THABIT MADAI, ZANZIBAR- MATUKIO DAIMA APP


SHIRIKISHO la soka Visiwani Zanzibar limekanusha Madai yaliyotolewa na Timu ya Wanawake ya New Generation kwa kushwandwa kuwasaidia baada ya kukwama njiani kutokana na kuishiwa fedha wakati wakitoka Nchini Uganda kushiriki Mashindano ya Afrika Mashariki na Kati kwa Timu za Wanawake CECAFA.


Timu ya Wanawake ya New Generation ilisambaza kwenye Mitandao ya Kijamii taarifa iliyotolewa na Nahondha wake, Warda Abdulhakim Mwinyi wakidai kukwama Mkoani Geita kutokana na kudaiwa na Dereva wa Gari ambalo walikuwa wanalitumia kusafiri nalo kutoka Uganda hadi Tanzania.


Aidha kupitia taarifa ambayo ilitolewa na Timu ya New Generation walidai kuwa baada ya kukwama Mkoani Geita walifanya jitihada za kuwasiliana na Shirikisho la Soka Visiwani Zanzibar na kushindwa kupatiwa Msaada unaostahiki.


Akizungumza leo na Waandishi wa Habari Rais wa Shirikisho la Soka Visiwani Zanzibar Suleiman Mohammed Jabir amekanusha Taarifa zilizotolewa na Timu hiyo na kudai kuwa Uongozi wa Shirikisho hilo umeshindwa kuwapokelea Simu kwa ajili ya kutoa Msaada ambao unahitajika.


Rais wa Zff amesema kuwa, Shirikisho la Soka Zanzibar liifanya jitihada za kuwasiliana na Timu hiyo kabla na baada ya safari na hawakupokea simu kutoka kwa Timu ikiwaeleza kuwa wamekwama hadi pale ambapo walioona taarifa zinaenea katika mitandao ya kijamii.


"Ndugu Waandishi wa Habari kwanza napenda kukanusha kuwa Uongozi wa ZFF haukupokea Simu kutoka Timu ya New Generation hata hivyo Siku ya jana Jumapili katibu wangu anapoishi ni maeneo ambayo yanasumbuliwa na Mitandao," amesema Rais wa ZFF.


Hata hivyo ameeleza Kuwa, Uongozi wa ZFF haukutoa ahadi yoyote kwa Timu hiyo ya New Genetation wakati wanapokwenda kwenye Mashindano ya Vilabu kwa Timu za Wanawake.


"Baada ya kadhia hiyo kupitia Uongozi wa ZFF umefanikiwa kutoa Laki Tano siku ya Jana kwa Timu hiyo na kukanusha Taarifa zinazodai kuwa Kiasi hicho cha Fedha kimetolewa na Timu ya Geita Gold," Amefafanua.


Aidha Ameifafanua kuwa, Tayari wameshakamilisha taratibu zote na kulipa Deni ili timu hiyo iweze kusafiri hadi Zanzibar bila changamoto yoyote ile.


Timu ya New Generation walianza Safari ya Kurudi Visiwani Zanzibar Siku ya Jumamosi ambapo walipofika Kahama walikwama kwa madai ya Dereva uishiwa Mafuta ya kuwafikisha Dar Es Salaam ambapo Timu hiyo ilishindwa kumalizia kiasi cha fedha ambacho waliahidiana.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI