Na Amina Said - Matukio Daima App, Tanga.
Wananchi wametakiwa kujiwekea utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara badala ya kungojea mpaka waugue kwani itaweza kuwasababishia gharama kubwa ya kujitibia
Hayo aliyasema leo Waziri wa afya Ummy Mwalimu wakati akizindua kambi ya upimaji bure wa magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza ambayo yataendeshwa kwa siku tano na Taasisi ya Afya Check kwenye viwanja vya Usagara mkoani Tanga ambapo zaidi ya wananchi 1000 wamejitokeza kufanya vipimo hivyo vinavyotolewa
Aidha aliwataka watu wajitokeze pale wanaposikia tangazo la kuchunguzwa afya zao kwani wanaweza kujitibia kwa gharama kubwa lakini utakuta matibabu ni bei nafuu na usipojua afya yako mapema iatakugharimu kutoa fedha nyingi hivyo ukijua unakisukari unatibika endapo utafuata ushauri juu ya kuacha vitu ambavyo ni visababishi
Pia alitaja baadhi ya vyakula vinavyotumiwa na watu kwa wingi na kwa mazoea pamoja na sukari au kula chumvi kupitiliza
Kwa upande wake Mratibu wa taasisi ya Afya Check ,Dr Isack Maro alisema katika siku tano watakazoendesha zoezi hilo mkazo mkubwa utawekwa katika magonjwa ysiyoambukiza ambayo .ni pamoja na mgonjwa ya pesha,kisukari,tezi dume na shinngo shingo ya kizazi alisema kuwa kwa siku ya kwanza tu zaidi ya wananchi 1000 wamejitokeza
"Kwa hali hiyo inaonyesha huenda idadi ya watu watakao hudumiwa watafikia zaidi ya elfu tano" alifafanua Dr.Maro
0 Comments