Header Ads Widget

WANAFUNZI NJOMBE WAONYWA JUU YA UKIUKWAJI WA MAADILI

 


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Mdhibiti ubora wa elimu kanda ya nyanda za juu kusini Marry Msongolwa amewaonya wanafunzi mkoani Njombe kutojiingiza kwenye vitendo vya ukiukwaji wa maadili vitakavyowasababishia kufukuzwa shule na kuharibu maisha yao.


Msongolwa ametoa onyo hilo wakati akizungumza na wanafunzi wa Mtwango sekondari wilayani Njombe wakati mkuu wa mkoa wa Njombe alipo zulu shuleni hapo na kwamba atakayekwenda kinyume na maadili ya kitanzania atachukuliwa hatua za kisheria.



Aidha mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka amesema anataka kuona wanafunzi wote katika mkoa wake wanasoma huku wakizingatia maadili mema na kwamba suala la nidhamu ndilo litakalo wafikisha kwenye mafanikio.


Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Christopher Sanga ameahidi kutoa zawadi kwa wanafunzi watakaofanya vizuri katika mitihani yao ikiwa ni motisha ya juhudi zao katika masomo.



Baadhi ya wanafunzi wa Mtwango Sekondari akiwemo Gladness Mgaya na Jackson Elia wameiomba serikali kuendelea kuwasaidia kutatua changamoto zinazowakabili shuleni hapo ikiwemo ya maji.






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI