Header Ads Widget

WAKUU WA MIKOA NA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA SHUGHULIKIENI MALALAMIKO YA WANANCHI KWA WAKATI - DKT. MPANGO



Na Scolastica Msewa, Kibaha


Makamu wa Rais Dr Phillip Mpango amewataka Wakuu wa mikoa na Makatibu tawala wa mikoa nchini kushughulikia kwa kutatua kero za malalamiko ya Wananchi kwa wakati badala ya kuacha hadi wakaanza kupaza sauti wenyewe wakitafuta utatuzi wa kero zao ngazi taifa.


Amesema hayo mjini Kibaha wakati akifungua Mafunzo ya wiki moja ya uongozi kwa Wakuu wa mikoa na Makatibu tawala wa mikoa Tanzania bara yaliyofadhiriwa na Bank ya NMB kwaagizo la Mheshimiwa Rais Dr Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kuboresha, kuongeza stadi kazi na ujuzi wa utendaji kazi katika kumsaidia Rais kuhudumia Wananchi.


Alisema kumekuwa na kuchelewa kwa utatuzi wa migogolo wa Wananchi ambako hupelekea Wananchi kupaza sauti zao wao wenyewe kwa kupeleka malalamiko ya ngazi za juu wenyewe.


"Kumekuwa na kutokujibu barua za Wananchi na Viongozi kutatua kero zao kwa wakati jambo ambalo hupelekea wao wenyewe kutafuta utatuzi wa kero zao ngazi za juu" alisema.


Alisema pamoja na mambo mengine Mafunzo hayo sio mapya lakini yatawawezesha kuelewa dhana ya usiri katika uendeshaji Serikali na wajibu wao katika udhibiti uvujaji wa siri za Serikali na pia wawe na ufahamu wa masuala ya msingi yanayohusu ulinzi, usalama wa nchi na 


Alisema ni muhimu Viongozi hao kufahamu utendaji wa serikali za mitaa na serikali kuu jinsi inavyohudumia Wananchi pasipo muingiliano wala migogolo.


Alisema ni vema kwa viongozi hao wakitambua dhana na uelewa wa msingi katika kuzingatia dhamana waliyopewa na Mheshimiwa Rais katika kuwahudumia Wananchi na katika kudhibiti utoaji wa siri za serikali katika uendeshaji wa serikali hasa kipindi hiki cha uwazi na maendeleo ya utandawazi wa mawasiliano.


Alisema ni muhimu kuwa na ufahamu mzuri wa masuala ya msingi yanayohusu ulinzi na usalama katika nchi yetu na hasa juu ya usimamizi makini wa rasilimali za nchi yetu ikiwemo rasilimali watu na rasilimali fedha katika kutekeleza miradi ya Maendeleo.


"Mafunzo haya ni muhimu kwa kuongeza ufanisi wa utendaji katika kuwahudumia Wananchi na kuongeza tija na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yenu kwa Wananchi" alisema Dr. Mpango.


"Mafunzo ni fulsa kwenu katika kuongezea uzoefu wenu hususani siri za uzoefu wa mikoa yenu kwani mada zote ni nzuri na muhimu katika kuboresha utendaji wenu na dhima ya Mafunzo hayo ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 inayoelekeza umuhimu wa utendaji shirikishi na Wenye ubora na katika ibala ya 122( a) ya Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020 ambayo inawaelekeza Wakuu wa mikoa kupata Mafunzo ili kuboresha utendaji wenu wa kazi" alisema.


Aidha aliyataja mapungufu na malalamiko ya utendaji katika baadhi ya mikoa nchini kwa kutokuzingatia mipaka kati ya Wakuu wa mikoa na Makatibu tawala wa mikoa hasa kuingiliana majukumu ya usimamizi wa fedha ikiwa ni pamoja na ubabe na unyanyasaji wa kingono na ucheleweshaji wa upandishaji wa vyeo kwa baadhi ya Watumishi.


Alisema sababu za Mheshimiwa Rais kuagiza Mafunzo hayo kwa viongozi hao wa mikoa nchini kuwa ni kutokana na kuwepo kwa mapungufu wa kiutendaji kwa viongozi hao.


"Yapo mapungufu ya kiutendaji katika mikoa ambapo kuna Usimamizi hafifu wa miradi ya Maendeleo na kutosimamia ipasavyo ukusanyaji wa mapato lakini pia yapo malalamiko kutoka kwa Wananchi wa mikoa mnayoiongoza" 


Aidha aliitaja baadhi ya mifano ya upungufu wa kiutendaji kuwa ni pamoja na kuwepo kwa kutokuzingatia mipaka ya kiutendaji katika ya Wakuu wa mikoa na Makatibu tawala wao ambayo ni kinyume cha taratibu, sheria na kanuni zilizopo ambayo hutokea sana upande wa fedha kwa baadhi ya Wakuu wa mikoa wanataka wahusike na masulufu.


 "Pia tunaona kushindwa kudhibiti na utunzaji wa siri za serikali mambo ambayo hayatakiwi kutoka unayakuta kwenye mitandao"


" Hatahivyo tunaona mahusiano mabaya kati yenu na Watumishi wa chini yenu upendeleo katika michakato ya upandishaji wa vyeo pamoja na mahusiano mabaya baina yenu na Watendaji wengine wakiwemo Viongozi wa Chama, wabunge, viongozi wa Taasisi mbalimbali, Wakurugenzi wa miji na majiji, madiwani na vyombo vyingine kama TAKUKURU" alisema Mheshimiwa Mpango.


Akizungumzia uwekezaji nchini amesema jitihada mahususi za kuvutia wawekezaji bado zinahitajika nchini sambamba na kuongeza ushirikiano na wawekezaji walio katika mikoa yao.


Mheshimiwa Dkt. Mpango alitoa msisitizo kwa viongozi hao kuzingatia maadili na nidhamu katika maeneo yao ya kazi kwa utendaji wa kupeleka Maendeleo kwa Wananchi.


"Sikilizaneni, jadilianeni katika mafunzo yenu haya na msisite kuleta mapendekezo yenu katika maadhimio mtakayojiwekea na mtakachofundishwa mpeleke kwa walio chini mnaowaongoza" 


Msimamie wasisitize utunzaji wa mazingira na kutangaza fulsa zilizo katika utunzaji wa mazingira katika mikoa yao" alisema.


"Jitahidini kusoma na kuelewa zaidi sheria, Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020, mpango wa Maendeleo wa mwaka 2020 /2025 na dira ya Maendeleo" 


Awali akimkaribisha Makamu wa Rais huyo Waziri wa Ofisi ya nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Angellah Kairuki alisema Mafunzo hayo ya wiki moja Wakuu hao wa mikoa na Makatibu tawala wa mikoa watafundishwa masomo 20 na wawezeshaji wabobezi waliowahi kufanya kazi serikalini kwa muda mrefu.


Alisema tayari mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji Makatibu tarafa yanaendelea ambapo wanafundishwa kwa awamu kwa kugawanyishwa kwenye Kanda za mikoa nchini Hadi watakapo kamilika wote nchi nzima.


Naye Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais menrjimenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora Ridhiwani Kikwete amesema mafunzo hayo yatasaidia kuboresha wa Umma na Utawala Bora katika mikoa nchini.












Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI