Na Johnson Jumanne, Matukio Daima App.
Kuhusu Haruna Niyonzima ni mchezaji wa Simba ukiona ndege imetua hapa na wachezaji ujue ndani yupo Haruna Niyonzima au anaweza kuja mapema kabla ya timu.
Yalikuwa ni maneno ya Asifa habari wa Simba Haji Manara wakati huo kuhusu usajili wa Haruna Niyonzima kwenye kikosi cha Simba. Nataka turudi nyuma ya muda mtu wangu.
Kuna misimu 6 ndani ya Yanga, Haruna Niyonzima alitufunza maana halisi ya kiungo mchezeshaji. Alitoa kila kitu kwenye eneo la kiungo, Nani hakufurahi uwepo wa Haruna Niyonzima.
Sura ya upole,busara nyingi. Alituonesha namna ya kupiga pasi za aina zote. Alikuwa dobi kweli, Hakuna mwana Yanga asiyemjua. Hakuna mpinzani ambaye hakuwa kumuhofia, Ndio aliitwa Fabregas.
Hadithi zangu zinanipeleka pale Misri Yanga wanapiga mpira mwingi dhidi ya Al Ahly kwenye dimba la Borg El Arab pale Alexandria.
Usiku ule Al Ahly wanapata goli la ushindi dakika za gizani Yanga walicheza kwa kujitoa sana, Haruna Niyonzima alikuwa kioo cha Yanga.
Kwenye Yanga ile ya mdachi Hans Van Der Pluijm, Haruna alikuwa na kazi kuipelekea timu kwa Thabani Kamusoko na ilifika, Akaivusha hadi kwa Simon Msuva bila kukosea.
Mbwembe za aina zote, Alikuwa kachumbari kwenye pilau, Pasi za mateso, Aliondoka Yanga na kuacha hadithi nzuri na za kuvutia.
Bado Simba hawajaisahau ile sub yake chini Patrick Aussems, Aliingia kiwanjani Mnyama akiwa anatafuta matokeo ya kushinda tu. Tayari maarifa ya Okwi yalifika kikomo.
Haruna alikwenda kiwanjani kama Game changer, Alichukua timu kwa James Kotei akaipeleka kwa Clatous Chama. Akaihamisha kwa John Boco kilichokuja kutokea ni historia tu.
Ukifika pale Rio de janeiro kuna hadithi nyingi za fundi Philippe Coutinho kitasa Thiago Silva. Full back left Marcelo bado kuna hadithi za namba 9 bora zaidi kuwahi kutokea ulimwenguni Ronaldo De Lima.

Sogea hadi Mogi Das Cruzes utawaambia nini na Neymar wao, Lakini pale Gisenyi Rwanda bado hawasahau uzao ule wa Haruna Niyonzima.
Nchi ilipata bahati kushuhudi kipaji kikubwa cha Haruna Niyonzima, Rudi katizame tena mechi ya Simba dhidi ya Sevilla na majibu baki nayo, Ndio ni Haruna Niyonzima Fabregas.



.jpeg)





0 Comments